TANGA RAHA (38)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Rahma akaanza kunitekenya huku akizungumza kwa sauti ya kudeka,nikajikuta nikicheka ila kusema ukweli moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo,kwa bahati mbaya katika kumi-nyana minyana na Rahma nikamkwaruza kwenye mkonoSASA ENDELEA...
“Baby kucha zako ndefu ngoja nikachukue kiwembe nije nikukate”
“Kiwembe wewe umekiona wapi?”
“Kuna kimoja nilikiweka kwenye wallet yangu ndogo”
Rahma akaelekea chumbani na mimi nikaendelea kujilaza kwenye kochi na baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa na wallet yake na akaifungua nikaona kadi nyingi za benki
“Makadi yote hayo ya benki ni ya nani?”
“Nimechukua kadi ya baba,mama na zangu na zote ninazijua namba zao za siri.....Mungu akibariki tukirudi hivi nataka tokatoe pesa zote kwenye akaunti zao kisha twenda mbali na hapa”
“Unataka twende wapi?”
“Oman popote ambapo tunaweza kwenda kupata uraia wa kutuwezesha kuishi kwa amani na furaha katika maisha ya ndoa yetu”
Rahma alizungumza huku akiendelea kunikata kucha taratibu mkono wa kulia
“Ahaa mume wangu una kucha nzuri”
“Mmmm umeanza”
“Sio nimeanza kwani mtu kumsifia mume wake ni vibaya kama hutaki unamakucha mabaya ka-ma zombie”
“Ahaa haya bwana kama mimi zombi basi wewe mama zombi”
“Jamaani baby....”
“Hakuna cha jamani tena wewe mazombi yake yanayo fanya khaa”
Nilipo kuwa nikijitingisha nikimuonyesha Rahma jinsi ya aina ya mazombi anayo fanana nayo kwa bahati mbaya akanikata kwenye kidole na damu zikaanza kunimwagika
“Umeona sasa na kuigiza kwako uzombi umejitingisha hadi nimekukata”
“Hembu nenda kaniletee kitu cha kuizuia hii damu kutoka”
“Ila pole mume wangu”
Rahma akanibusu kwenye uso na kuingia jikoni na mimi nikabaki nikiwa nimejishika kidole huku damu zangu zikimwagikia kwenye sakafu iliyo tengenezwa kwa mbao ngumu sana.
Akarudi akiwa ameshika pakti ya chumvi na bakuli lenye maji.Akaanza kuninawisha taratibu kisha akanipaka chumvi ya kutosha ili kuizuia damu isitoke kwa wingi
“Eddy hiyo pete amekuvalisha nani?”
“Nimevaa tuu”
“Sipendi nakuomba uivue”
“Baby hii si ninapendeza nikiivaa”
“Sitaki ninakuomba uivue kwa maana pete yangu ndio inapaswa nikuvalishe ila sio wewe kujivalisha mapete pete yako ya ajabu”
Rahma alizungumza kwa hasira huku akiushika mkono wangu wa kushoto na kuanza kuicho-moa pete,
“Babay ila hiyo pete ni ya dawa”
“Kwenda zako huko tangu lini pete zikawa dawa......au umevalishwa na mwanamke wako huko unajidai ni ya dawa”
“Sio hivyo baby ila kuna...”
“Sitaki kusikia cha kuna wala nini....Hivi Eddy mashani mwako umesha wahi kupata mwanamke ambaye yupo tayari kujitoa maisha yake kwa ajili yako?”
“Hapana?”
“Kwa hiyo mimi nilikuwa mjinga sana kusimama mbele yako ili risasi inipate mimi si ndio?”
“Hapana mpenzi wangu ninakuomba upunguze jazba....hiyo pete mimi nimeivaa kutokana na matatizo yangu binafsi na kuna dada mmoja ndio alinipatia ili nijikinge nayo”
“Dada ehee dada eheee....kwahiyo mukavalishana?”
Rahma alizungumza huku machozi yakimwagika taratibu na akanyanyuka kwa hasira na kutoka nje akiwa na pete yangu mkononi na mimi ikanibidi nitoke nje kumfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye moja ya mabembea yalipo kwenye bustani za hili jumba
“Rahma”
Nilimuita huku nikimshika mkono na akaitoa mikono yangu kwa hasira
“Eddy sitaki uniguse nakuomba uniache”
“Siwezi kukuacha kwa sababu wewe ni mpenzi wangu”
“Eddy mimi sio mpenzi wako na unikome na kuanzia sasa hivi Eddy ninakuapia sitaki kuwa na wewe tena.....Mimi napigwa risasi na baba yangu kwa ajili yako,ninawakimbia wazazi wangu kwa ajili yak oleo hii unanimbia eti kuna mwanamke alinipa eti nijikinge unadhani mimi ni mtoto mdogo kiasi cha kunidanganya”
“Rahma mke wangu nakuoma uniamini hiyo pete mimi inanisaidia kuona mauza uza yanayo nitokea usiku”
Nilizugumza kwa sauti ya uyonge na ya upole ila sura ya Rahma haikubadilika na kwajinsi ni-navyo mjua Rahma hasira yake huchukua mud asana kuondoka
“Eddy hivi unajua ni dhamani gani ambayo mimi ninakupa,unajua ni jinsi gani mimi ninavyo kuchukulia wewe kama kiongozi wangu wa maisha.....ila kwa nini unafanya hivyo lakini?”
“Mke wangu ninakuomba unisamehe kama nitakuwa nimekuudhi kwa hilo ila kusema kweli hiyo pete mimi sina nia nayo mbaya kama unavyo nichukulia ila ukweli ni kwamba kuna majini yananisumbua sana usiku yanapelekea ninashindwa kuishi kwa amani mke wangu ninakuomba unipatie hiyo pete”
“Ahaa basi na mimi ninataka niyaone yakikusumbua na nikama pete yako nimesha itupa”
“Haaaa wapi...!!?”
“Sijiu na niankuomba uniache”
Ni kweli mikono yaRahma haikuwa na pete yangu mkoni na nikaanza kuitafuta katia sehemu ambayo Rahma amekaa ila sikuiona
“Mke wangu niambie basi ni wapi umeitupa?”
“Si nimekuambia usinihusi na mambo yako nenda kamuulize huyo Malaya wako aliye kupa akuchongeshee nyingine”
“Rahama usizungumze hivyo utanikasirisha”
“Kasirika kwani nimekuzuia kukasirika wee vipii”
Nikaachia msunyo mkali na kuendelea kuitafuta ni wapi ilipo na kwa dharau Rahma akanyanyuka na kuingia ndani,Sikufanikiwa kuipata pete baada ya kuitafuta kwenye kila sehemu ambayo nilihisi kuwa anaweza kuitupa,Nikarudi ndani sikumkuta
Rahma sebleni,nikaingia chumbani na kumkuta akiwa amekaa kitandani huku akiwa ameukumbatia mto machozi yakiendelea kumwagika hadi sura yake ikatawaliwa na uwekundu fulani.Akanitazama kwa jicho kali hadi ninakaa kitandani akaendelea kunitazama
“Mke wangu hembu niambie ni wapi ilipo hiyo pete”
Rahma hakunijibu zaidi ya kuendelea kunitazama na machozi yakazidi kumtoka,gafla nikastukia akianza kunipiga na mto alio ushika
“Eddy kwanini kwanini unanifanyia mimi hivi.....?”
Rahma aliendelea kunipiga na mto wake anaona haitoshi akantupa na kuanza kunipiga kwa mi-kono yake huku akiwa amenikalia kiunoni huku nikiwa nimejilaza chali.
Nikawa na kazi ya kui-zuia mikono yake isisiendeleaa kunipiga kwani nilimuachia apunguze hasira zake kwa namna hiyo ya kunipiga,Taratibu akaanza kupunguza nguvu na kasi ya kunipiga na taratibu akajishusha na kulilaza kichwa chake kwenye kifua changu na kuendelea kulia kwa sauti ya kudeka
“Eddy”
“Naam”
“Unanipenda?”
“Ndio ninakupenda mke wangu tena zaidi ya kukupenda”
“Kwa nini unanisaliti?”
“Mke wangu sijakusaliti na siwezi kufanya hivyo ndio maana niliamua kuja kukuchukua kwenu japo baba yako alinitena na kuninyanyasa kutokana na weusi wangu na kuto kuwa kwangu na pesa”
Nilizungumza kwa sauti ya uchungu huku machozi yakinilenga lenga
“Rahma nipo tayari kufa kwa ajili yako....alama zote za mistari niliyo chanwa na kisu yote ni kwaajili yako,Damu yangu nyigi ilimwagika kwa ajili yako.
Baba yako alitaka kunizika hai ila kwa uwezo wa Mungu nikafanikiwa kuokoka laity ingekuwa ni mtu mwengine angakuja kwenu tena eheee...?”
“Eddy ninakuomba unisamehe mume wangu najua ni jinsi gani unanipenda na kunihita-ji,natambua umeteseka kwa ajili yangu”
Rahma alizungumza huku akinifuta machozi ambayo yalisha anza kunimwagika,Rahma akaishusha midomo yake na kuikutanisha na midomo yangu na ndani ya dakika chache tukajikuta tukiingia kwenye dimbwi kubwa la mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake kwa jinsi anavyo jua yeye mwenyewe.
Tukamaliza na kuingia afuni huku nikiwa nimembeba Rahma,tukaanza kuoga na kurudi chumbani na kujitupa kitandani
“Eddy unataka kula?”
“Nimeshiba mke wangu au wewe una njaa?”
“Hapana nilitaka kujua kama unanjaa basi tutapika jioni”
Masaa yakazidi kukatika huku na jjioni tukasirikia kupika chakula cha usiku na tukala kwa pa-moja huku tulilishana na tukamaliza na sote kwa pamoja tukajilaza kwenye kochi moja
“Baby hivi ile pete uliitupa wapi?”
“Umesha anza unataka nikasirike eheee”
“Basi yaishe mke wangu kwa maana ukianza kukasirika utaanza kurusha makofi yako”
“Yaa kama Sensia vile”
“Toka huko Sensia uwe wewe umelegea hivyo”
“Nimelegea wapi wakati nimekupiga zakichina china”
“Hahaaa haya mwaya mke wangu ila na wewe ni baunsa”
“Twende tukalale ninahisi usingizi”
“Zima taa za sebleni”
Sote tukaingia ndani na kujilaza kitandani,usingizi mzito ukanipitia nakulala fofofo.Kwa mbali nikaanza kuhisi ngoma kubwa ikipigwa na watu wakishangilia.
Kwa mara ya kwanza nikaipote-zea nikijua ni ndoto zangu za kawaida,ila kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi sauti za watu na mlio wa ngoma hiyo ulivyo zidi kuongezeka kupigwa.
Nikachukua mto na kujiwekea kichwani na kuziba masikio ila nikahisi kitu na kujikuta nikikurupuka na pembeni yangu siku-muona Rahma.
Na mlio wa ngoma nikausikia ukizidi kuongezeka ilanibidi nichungulie dirishani ila sikuona watu wanao cheza ngoma hiyo kwa maana dirisha la chumba chetu linaelekea kwenye bustani ya nyuma
Nikaingia bafuni na sikumuona Rahma ikanilazimu kujifunga taulo na kwenda sebleni ambao mlio wa ngoma na kelele za watu zikazidi kuniumiza masikio yango.
Taratibu nikafungua pazia la dirisha la sebleni na nusu nipoteze fahamu ila nikajikaza kuendelea kutazama.
Kundi kubwa la watu wenye asili ya kijerumani wamewazunguka Rahma na jamaa mmoja wa kizungu huku Rahma akiwa amevalia shela la harusi huku na jamaa suti ya harusi na
Rahma ameishika pete yangu aliyo itupa akitaka kumvalisha jamaa kwenye kidole kama nilicho kuwa nimekivaa mimi na nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muongozaji wa harusi hiyo akiwa ni Olvia Hitler
Taratibu nikalifunga pazia na kukaa kwenye kichi huku nikijiuliza ninacho kiona ni kwelia au ni ndoto,Kelele za ngoma zikanifanya niweze kuamini kama ni kweli kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuufungua mlango na kuwafanya watu wate waliopo kwenye eneo nje kunitazama kwa macho makali ambayo si ya kawaida kama ilivyo kwa sisi binadamu.
Macho yao yametawaliwa na rangi ambazo si za kawaida kwa haraka haraka ninaweza kuzifananisha na mwanga wa moto wa gesi.
Rahma akabaki akinishangaa kama mtu asiye jitambua aliye kamatwa na bumbuazi kali,Nikaanza kupiga hatua mbili mbele na kuwafanya vijana wawili wa kijerumani kusimama mbele yangu na kunitazama kwa umakini kisha nao wakaanza kunisogela huku taratibu wakianza kubadilika maumbo yao kwa kutoka manyonya kama ya mbwa.
Nikaanza kurudi nyuma kwa haraka na nikausukuma mlango ila kwa bahati mbaya nikaukuta mlango ukiwa umejifunga kwa ndani.
Jamaa wakazidi kunifwata na sikuwa na jinsi zaidi ya kaanza kupiga hatua za hakanyaga maua yaliyopo pembezoni mwa ukuta na kuanza kukimbia kuelekea sehemu yenye msitu,Vijana wa kijerumani naa wakanza kunikimbiza na kadri wanavyo kimbia ndivyo miili yao ikabadilika na kuwa kama mbwa aina ya Bweha(FOX) na kuzidi kunikimbiza.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni