SORRY MADAM (58)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
ILIPOISHIA...
{HABARI YAKO BWANA EDDY, GARI YAKO IPO KWENYE WAKATI MGUMU WA USALAMA.KAMA UNATAKA ULINZI MINYA HAPA AU UNAWEZA KUKATA}NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikaminya sehemu yenye alama ya tiki(pato).Sikushangaa sana kwa maana hili gari aina ya BMW 007 limetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na ninakumbuka Sheila aliniambia kwamba amepewa na Wamarekani weusi alio cheza nao filamu ya ngono.Gari ikaanza kurudi chini kidogo kisha vioo vyote kasoro cha mbele vikapitiwa na ukungu mweusi ambao sikujua ni wa nini.
Kwenye kioo kidogo nikaona gari la mbele na la nyuma,nikaonyeshwa jinsi zivyo ndani na idadi ya watu waliomo ndani wakiwa katika hali ya mifupa(mafuvu).Nikiwa ninashangaa shangaa nikastukia nikigongwa na gari ya nyuma na kunifanya nishindwe kulizuia gari na likamgonga gari la mbele.
Nikastukia kuona jamaa wawili kwenye gari la mbele wakichomoza kwenye vioo vya pembeni na kuanza kunishambulia kwa kutumia bunduki zao,Kitu kilicho nistaajabisha ni jinsi risasi hizo kushindwa kuingia ndani ya gari langu.Nikaanza kujiamini kuwa gari yangu imepata kweli ulizi,Nikakanyaga breki za gafla na kusababisha gari la nyuma kunigonga na kuanza kuzunguka barabarani kwa kasi na kuacha njia na kuvaamiti iliyopo pembezoni mwa barabara na kupinduka.Nikaachia breki na kulifukuzia gari la mbele ambalo kidogo liliniacha kutokana na mwendo wao wa kasi,Nikalisogelea kwa ukaribu,kila ninapo jaribu kulipita wananizuia.Nikaongeza mwendo,kutokana na gari yangu kuwa chini kidogo likaweza kupiga tairi za nyuma na kulifanya linyanyuke kidogo na dereva wake kushindwa kulimudu na kuanguka vibaya na kuanza kubingirika likiingia msituni.
Gari la mbele likapunguza mwendo na kutokana lipo mbali kidogo na mimi, likafunga breki za nguvu na kwa utaalamu mkubwa dereva wa gari hilo aliweza kuligeuza na likawa limegeuka nilipo mimi.Nikapunguza mwendo hadi nikasimama mita chache kutoka lilipo gari langu.Derevaa wa gari lililopo mbele yangu akaanza kuvuta mafuta huku akiganyaga breki na kuzifanya tairi za gari lake kuzunguka kwenye lami pasipo kwenda mbele na kuzifanya zitoe mlio fulani.Nikazima taa za gari langu na dereva akazima za kwake.Nikawasha za kwangu ila nikajikuta nikinshangaa dereva wa gari hilo kwani anafanana sana na Manka japo simuoni vizuri ndani ya gari hilo.Gafla nikalishuhudia roli linalo malizia kona iliyopo karibu na lilipo simama ‘Hammer’,Sikujua kama dereva wa Hammer ninaye mfananisha na Manka kama ameliona lori hilo au la kwani anaendelea kuzifunga breki za gari lake katikati.Nikazisika honi za lori zikimuashiria dereva wa Hammer kuondoka barabarani,ndani ya sekunde kadhaa nikastukia kuona lori likiligonga kwa nyuma Hammer na kulisogeza pembeni ya barabara na lori likapita pasipo kusimama.
Ukimya ukatawala kesemu nzima,nikataka kuondoka ila nikataka kujua niliye muona ni Manka kweli au sio yeye.Nikalisimamisha gari pembeni,nikaichomoa bastola yangu,nikafungua mlango na kushuka ndani ya gari.Nikatazama pande zote za barabara hapakuwa na gari lolote linalo kuja.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari hadi sehemu lilipo anguka gari la watu ambao ninahisi sio watu wazuri.Nikalisogelea taratibu.Nikachunguza ndani na kumuona mtu moja aliye kaa pembezoni mwa dereva akiwa amekitwa na kisiki cha mti kwenye kichwa na amefariki hapo hapo,Siti za nyuma zilijaa maboksi makubwa na hapakuwa na mtu wa aina yoyote.Dereva wa gari ambaye ni mwanamke aliendelea kujitahidi kutoka ndani ya gari pasipo kugungua kama mimi nipo eneo hilo.Akasimama huku nywele zake nyingi zikiwa zimemfunika usoni mwake,akakutana na mdomo wabastola yangu.Akajiweka nywele vizuri na nikahakikisha ni Manka kwani akawa ni wakwanza kuliita jina langu
“Eddy”
“Naam”
Tukakosa cha kuzungumza,Uvaaji wa Manka unaashiria kuwa ni jambazi kwani kuanzia juu hadi chini amevaa nguo nyeusi tupu zinazo endana na nguo za jeshi.Mikono yake amevaa gloves nyeusi.Kifuani amejifunga jaketi la kuzuia risasi(bullet proof).Kiunoni mwake anabastola mbili zilizo chomekwa kwa kwenye kiuno
“Umeumia?”
“Hapana”
“Tuondoke”
“Hapana ngoja kuna kitu tusaidiane”
“Nini?”
“Kutatoa haya maboksi”
Sikutaka kuuliza yana nini zaidi ya kusaidiana kwa pamoja kuyatao maboksi mawili makubwa kiasi.Kwa uzuri yakaingia kwenye gari langu siti ya nyuma.Manka akachomoa bastola yake na akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuftatua risasi kazaa kwenye tanki la mafuta ya gari lao na likalipuka.Akaingia ndani ya gari langu na safari ikaendelea.Dakika kumi nzima ndani ya gari hakuna aliye msemesha mwenzake.
“Eddy usiku huu unakwenda wapi?”
“Arusha”
“Kuna nini?”
“Kuna ishu ninakwenda kufanya na wewe je?”
“Nitakuambia tukitulia”
“Boksi zina nini?”
“Pesa”
“Pesa.....!!?”
“Ndio”
“Za nani?”
“Ndio maana ninakuambia nitakuambia tukitulia”
Nikazidi kuongeza mwendo na ndani ya masaa mawili tukawa tumefika Arusha.Tukafika hadi kwenye mtaa wa wachaga na tukaingia kwenye moja ya nyumba iliyo tulia sana.Manka akashuka kwenye gari na kufungua geti na mimi nikaliingiza gari ndani akafunga huku akitazama pande zote kisha akalifunga geti.Akafungua mlango wa nyumba hiyo na tukayaingiza maboksi yote ndani.Tayari mwanga wa jua ulisha anza kuchomoza kwa mbali ikiashiria ni asubuhi
“Oya mimi ngoja nikapige mishe ninayo itaka kisha nitakustua”
Nilimuambia Manka ambaye alianza kukata biksi moja kwa kutumia kisu.Nikashuhudia vibunda vya elfu kumi kumi vikiwa vimejaa ndani ya boksi
“Nimeshatoka kimaisha mpenzi”
“Mmmm....”
Manka akanirushi kibunda kimoja cha pesa kuku vingine akivitoa na kuvirusha rusha juu kwa furaha.Manka akanifwata na kunikumbatia kwa furaha huku akinipiga mabusu mdomoni
“Eddy furaha yangu imekamilika sasa”
“Kwa nini?”
“Nina pesa na nimekupata wewe,nilikutafuta kwa siku nyingi mpenzi wangu”
Wazo la Manka kuwa ni dada yangu likanijia akilini mwangu.Nilipo kumbuka kuwa baba yake ni baba mkubwa nikakaa kimya pasipo kujibu chochote.
“Nikupeleke sehemu ambayo unataka kwenda?”
“Hapana”
“Twendwe wote bwana”
“Ila ubadilishe nguo zako”
“Unadhani sina akili,nilazima nibadilishe”
Manka akaniachia na kuingia kwenye moja ya chumba.Baada ya muda akatoka akiwa amejiremba na mtu unaweza kumsahau kama yeye ndie aliyekuwa akiliendesha gari la majambazi.Nikalitoa gari nje,akafunga geti lake,akaingia ndani ya gari nasafari ikaanza.Nikalisimamisha gari nje ya geti la madam Mery
“Hapa kama napajua?”
“Ni kwa mwalimu wangu mmoja”
“Namjua si yule Mery?”
“Ndio,ila nisaidie kitu”
“Kitu gani?”
“Ninaomba ukagonge”
“Alafu”
Nataka kuingiza gari humo ndani”
Manka akashuka kwenye gari na kuaza kugonga geti,dakika kama mbili gati likafunguliwa na Madam Mery.Wakasimuliana kwa furaha na madam Mery.Kutokana na kufunga vioo vya gari langu madam Mery hakuweza kuniona.Madam Mery akazungumza kidogo na Manka kisha akafungua geti na Manka akarudi ndani ya gari.Nikawasha gari na kuliingiza ndani.Manka akawa wa kwanza kushuka,nilipo hakikisha madam Mery amefunga geti na kuanza kwenda ndani kwake ndipo na mimi nikashuka.Madam Mery akastuka kuniona.Akataka kuingia ndani ila akakutana na John rafiki yangu akiwa amevaa kibukta akiwa tumbo wazi ikiashiria John na Madam Mery wanamahusiano ya kimapenzi.John akapigwa na bumbuazi kana kwamba anasubiria kupigwa picha ya mnato hii ni baada ya kuniona
Sikuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzunguka nyuma ya gari,nikafungua buti ya gari na kutaka kulitoa turubai lenye mwili wa Derick,nikafikiri kwa muda kidogo kisha nikalifunga buti pasipo kulitoa turubai
“John niaje?”
“Ahaa....ahaa powa”
John alinijibu kwa kubabaika nikabaki nikitabasamua na kumfwata Manka sehemu alipo simama
“Jamani,hamutukaribishi ndani?”
Niliuliza na kumfanya madam mery kushtuka,akatabasabu kiwoga huku midomo yake ikitetemeka akishindwa hata kuzungumza anacho taka kukizungumza
“Nd...aaaniii kar..ibu....ni”
Manka akabaki akiwa anashangaa kwani hali ya kuzungumza kati ya Madam Mery na John zilibadilika kwa kiasi kikubwa.Madam Mery akaongoza msafara wa sisi kuingia ndani kwake,mtu wa mwisho kuingia ndani nikiwa ni mimi.Nikaufunga mlango na kwabahati nzuri nikakuta funguo ya mlango ikiwa inaning’inia mlangoni.Nilipo hakikisha nimeufunga mlango nikaidumbukiza fungoa mfukoni mwangu na kukaa kwenye moja ya sofa.
“Madma kwako kumebadilika”
Nilizungumza kinafki kwani hapakuwa na mabadiliko yoyote tangu nilivyo paacha siku ya mwisho ninapambana na muwe ndivyo nilipo pakuta.Kikubwa kilicho badililika ni vitambaa vya makochi ni meza mpya ya kioo
“John,masomo yanaendeleaje?”
“Masomo kidogo yapo vizuri”
John alizungumza kwa sauti ya unyonge nayaupole sana,huku sura yake ikiwa inatisama chini kwa aibu anashindwa hata kunitazama usoni
“Sasa,ndio munaingia kidato cha sita?”
“Ndio”
“Hongereni”
Wakati ninazungumza na John.Madam Mery na Manka walikaa kimya wakitusikiliza.Macho yangu nikayahamishia usoni mwa madam Mery ambaye naye hakutaka kabisa kunitazama usoni
“Wenyeji mbona mumepooza gafla?”
Manka alizungumza na kuwafanya John na madam Mery kunyanyua nyuso zao na wakazipamba kwa tabasamu ambalo kwangu ninajua ni tabasamu lililo jaa aibu na ninavyo hisi kila mmoja anaomba ardhi ipasuke na immeze
“Haaa sisi,tunazungumza”
Madam Mery alizungumza manene ambayo kama mtu mzima mwenye akili zake hawezi kuzungumza pumba kama hizi kwa maana kwa muda wote yupo kimya kama amejaza fumba la uji wa bada(uji wa unga wa miogo)
“Ngoja nikawaandalie hata chai wageni wangu”
Madam Mery alizungumza huku akinyanyuka.Nikamtazama na kutingisha kichwa nikiashiri nimekubali akafanye kazi hiyo.
“Manka yule ni rafiki yangu anaitwa John,John huyu ni Manka ni zaidi ya ndugu yangu”
“Nashukuru kwa kumfahamu”
Manka akanyanyuka na kumpa John mkono kama wa kusalimiana kwa mara nyingine tena
“Mimi ngoja niende msalani”
“Sawa”
Nikanyanyuka na kuondoka sebleni na kuwaacha Manka na John.Nikapitiliza moja kwa moja hadi jikoni na kumkuta Madam Mery akiwa ameuegemea ukuta,akionekana kuwa katika mawazo makali na mazito yanayo mfanya ashindwe hata kutazama maji yanayo mwagika kwenye jiko la gesi,baada ya kuchemka sana.Hadi ninazima jiko ndio madam Mery anastuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo
“Unawaza nini?”
“Aahaa hakuna”
“Siku hizi unaniongopea hata mimi?”
“Eheee,”
“Ehee,unaisoma au unaiandika?”
“Tuachane kwanza na hayo,mume wako yupo?”
“Nimeachana naye?”
“Umeachana naye,kisa ni nini kilicho wafanya muachane?”
“Wee acha tuu.Ila kila kitu wewe unakijua?”
“Mimi,mbona kama sikumbuki?”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni