KIJIJINI KWA BIBI (41)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kayoza akatumia vizuri nafasi ya kumshambulia mfululizo mpaka Mkuu wa Polisi akawa hatamaniki kwa jinsi alivyokuwa anavuja damu kichwani, ghafla Mkuu wa Polisi akampiga teke Kayoza na kusababisha chupa imponyoke Kayoza, Mkuu wa Polisi kwa kasi ya mshale, akakimbilia katika kitanda chake, akaunyanyua mto, kisha akachukua bastola yake na kumuelekezea Kayoza,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"mwanaharamu mkubwa wewe, kwa kitendo ulichonifanyia, sio rahisi nikikuacha hai", Mkuu wa Polisi aliongea huku akikoti risasi katika bastola yake, Kayoza alitawaliwa na hofu na kukata tamaa. Aliamini hapo ndipo mbio za kupambana na Mkuu wa polisi zake zilipoishia.
Mkuu wa polisi akaweka target katika paji la uso wa Kayoza, Kayoza akafumba macho kuashiria kukata tamaa, Kisha Mkuu wa Polisi akafyatua risasi..
…lakini risasi haikutoka, Mkuu wa polisi akajaribu tena, lakini hali ikawa ile ile, bastola ilikua haina risasi, Mkuu wa Polisi akaruka mpaka kwenye kabati, akachukua mfuko wa risasi, Kayoza kuona hivyo, akaikimbilia chupa ya soda aliyokuja nayo, ambayo ilikuwa karibu na mlango, ile kuikota ili amuwai akakuta tayari Mkuu wa Polisi anaikoki bastola, Kayoza akamuwai, akarusha ile chupa ambayo iliupiga mkono wa Mkuu wa Polisi ambao ulikua umeshika ile bastola na kufanya ile bastola iende chini, Kayoza akaruka juu na kumpiga teke Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Polisi akadondoka chini, Kayoza akaiokota ile bastola na kumfyatulia Mkuu wa Polisi risasi zisizo na idadi mpaka akafa. Kisha hapo ndipo akakiri kuwa ana kosa sasa la mauaji, kwa maana ameua kwa kukusudia tofauti na anavyoua kipindi mzimu unapompanda.
Kayoza akaenda katika kabati na kuvunja kioo, akachukua kipande cha kioo, kisha akachukua ndoo iliyo mule ndani na kwenda sehemu ulipo mwili wa Mkuu wa Polisi, akaanza kuuchinja huku akikinga damu kwa kutumia ile ndoo, mpaka aliporidhika. Na kumbuka kipindi chote hicho alikuwa na kitambaa puani ambacho alikipulizia pafyumu kwa ajili ya kuzuia harufu ya damu ya aina yoyote ile.
Baada ya kufanya ukatili huo ambayo hakutaka kabisa kuujutia, Kayoza alicheka mwenyewe ndani ya chumba ambacho alifanyia mauaji na kisha Kazi kubwa ambayo ilimkabiri kwa wakati huo ikawa ni kutoka nje, maana watu walishajaa nje.
Akachukua kichwa cha Mkuu wa Polisi akakiweka ndani ya ndoo, kisha akaifunika ndoo, safari ya kwenda nje ikaanza, alipofungua mlango watu wote wakatawanyika, kwa maana waliamini Kayoza sio mtu wa kawaida kabisa, na ili kuwatisha zaidi, Kayoza akapiga risasi hewani, watu wakakaa nae mbali kabisa, nguo zote alizozivaa zilikuwa zimetapakaa damu, ila yeye hakuweza kuisikia harufu ya damu kutokana na kitambaa alichojifunga puani kwa ajili ya kuhofia mzimu kumpanda endapo harufu ya damu itapenya puani mwake.
Akatoka na ndoo yake mpaka kwao, huku akifuatwa na kundi la watu na waandishi wa habari walikuwepo, tena wengi walikuwa na furaha kwa sababu ya kupata habari itakayouza magazeti yao.
Njia nzima alikuwa akitembea huku kundi kubwa sana la watu likimfuata na kila mmoja akisema lake kutokana na ukatili ule waliokuwa wanaushuhudia mubashara, kwa maana vitu kama vile walishazoea kuviona katika filamu za watu wa mashariki mpwa dunia au kukutana navyo katika simulizi za wakina ALEX KILEO.
Alipofika kwao, akatoa onyo kuwa, mtu yeyote asimsogelee, na mtu ataekaidi amri, atampiga risasi. na kweli walimuogopa kwa maana Kayoza wa siku hiyo hakuwa na chembe za ubinadamu kabisa, hata sura yake ilidhihirisha hiyo kwa maana zile damu zilizomtapakaa mwili mzima na macho yake yalivyokuwa mekundu yalionesha hakuna hatari anayoiona mbele yake. Tayari alishaamua kuwa mnyama na aliona hiyo ndiyo bora ya kufanya kwa wakati huo.
Baada ya kufika kwao, Kayoza akaingia katika chumba chake akajifungia mlango kwa ndani, hapo ndipo alipodhamilia kufanya kama Maelezo ya mganga wa mwisho kumtembelea yalivyosema, akakumbuka kuwa mganga alisema kuwa njia ya kuundoa huo mzimu inaweza kugharimu na maisha yake, yaani maisha ya Kayoza, hata Sajenti Minja alipouliza ni njia gani hiyo? Mganga alijibu kuwa itabidi achinjwe kondoo alafu Kayoza awekwe katika kitanzi ili harufu ya damu itakapoingia puani kwa Kayoza ni lazima mzimu umpande, na hapo ndipo ile kamba ya kitanzi ivutwe na imnyonge kayoza, ni lazima kayoza ni lazima afe na mzimu ufe kwa maana mzimu hutegemea pumzi katika kutoka na kuingia katika mwili wa Kayoza.
Baada ya Kayoza kuyakumbuka maneno hayo, alijikuta akitabasamu, tabasamu la umauti lililokuwa linatoka pasipokuwa na furaha ila hasira zilizotokana na kukata tamaa ya kupata suluhisho la matatizo yake.
kisha akachukua kamba akaitundika juu na kuweka kitanzi, kisha akaweka stuli na kupanda juu, alafu akaifunua ile ndoo ambayo aliiwekea damu ya Mkuu wa Polisi, akakitoa kile kichwa na kukitupia chini ya kitanda, kisha akajifungua kile kitambaa puani, harufu ya damu ikampenya sawa sawa katika matundu ya pua yake, alivyoanza kuhisi dalili ya kupandwa na mzimu akaitupa ile ndoo, na kuitegua stuli, mzimu ukawa tayari umeshampanda, na kitanzi kikambana sawa sawa, Kayoza na mzimu wake, akaanza kupiga kelele kwa sauti ya ajabu, hali iliyofanya watu waliokuwa nje ya nyumba watawanyike.
Nje, kwanza ilipiga radi kubwa sana, huku ikifuatiwa na upepo mkali sana, mpaka nyumba zenye udhaifu zilianguka, alafu ikanyesha mvua kubwa sana ikiambatana na jua kali sana.
Kayoza ilimchukua kama dakika thelathini kuangaika juu ya kitanzi, mwishowe alitulia kimya kabisa, na ukawa ndio mwisho wa maisha yake na mzimu wake.
Polisi ndio walikuja kuvunja mlango na kuukuta mwili wa Kayoza unatoa moshi na ulikuwa mweusi sana kuashiria alikuwa anaungua, macho na masikio yalikuwa yametoboka, hakika kilikuwa kifo kilichosikitisha sana, kifo ambacho kilihitimisha urithi wa kimizimu katika ukoo.
Sajenti Minja alilia kama mtoto kutokana na yote aliyofanya katika kumlinda Kayoza na uhai wake, lakini ilikuwa kama bure, na mbaya zaidi aliyakumbuka maneno ya Kayoza ya jana yake, ambayo Kayoza alidai anataka sherehe ifanyike leo kwa sababu anataka kufanya jambo la kukumbukwa daima.
"kumbe jambo lenyewe ndio hili, umelifanya mapema sana mjomba, ungesubiri mjomba, kama ungesubiri nina uhakika uhai wako usingetoweka", Sajenti Minja aliongea mbele ya jeneza la Kayoza ambalo liliwekwa mbele ya watu kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Kayoza.
Mama Kayoza alianguka na kuzimia mara nne, kitendo ambacho kilisababisha apelekwe hospitali na ikagundulika mshtuko wa moyo.
Mambo ya maziko yalienda kama kawaida na kumalizika salama.
Kwa upande wa Mkuu wa Polisi, mwili wake ulizikwa na manispaa ya mkoa wa Kigoma kutokana na kutopatikana kwa kichwa chake ambacho Sajenti Minja alikificha makusudi ili kupoteza ushahidi na baada ya Siku alienda kukizika.
Uko kwao Shinyanga hawakupata taharifa yoyote, habari zilizotangazwa kwa wafanyakazi wenzake yaani polisi wenzie ni kuwa amepotea na hajulikani halipo.
BAADA YA MIAKA 3
Anaonekana Sajenti Joel Minja akiwa na familia yake, wakiweka shahada la maua katika kaburi la Mama Kayoza ambae alikufa mwaka mmoja uliopita kutokana na ugonjwa wa mshtuko wa moyo alioupata kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye kipenzi (Kayoza).
Sajenti Minja aliacha kazi kutokana na ulemavu alioupata, sasa hivi ni mjasiliamali ambae ana kampuni yake binafsi ya usafirishaji wa abiria, ambayo inamiliki mabasi, maroli, daladala na taxi. Mabasi yake ni maarufu sana katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Tanga, Yanaitwa GHOST MEMORY.
Ana mke na watoto wawili, wa kwanza anaitwa Kayoza, na wapili anaitwa Omari, ikiwa kumbukumbu kwa watu wake wa karibu.
MWISHO
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni