JICHO LA TATU (6)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
wale vijana wawili wakaja haraka...wakaanza kutoa ngozi moja moja.....lakini kijana mmoja akasema kwa lugha yao akimwambia yule yule kijana aliyewaita,,akimaanisha,,"utakuwa umeona vibaya hakuna mtu hapa.....wakarudisha haraka ngozi hizo.....kwa kuzipanga.
walipomaliza wakazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho.......
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Vida aliendelea kujificha lakini uzalendo ukamshinda kutokana na joto na harufu kali ya ngozi hizo za wanyama pia alianza kukosa pumzi..akakurupuka akanyanyuka huku akikohoa kwa nguvu....
sauti ya Vida ikasikika...vyema kila mtu aliweza kusikia sauti ya vida akikohoa.....
wakarudi haraka ndani ya chumba kile..wakamkuta Vida wakamsisitiza atoke aende kwa baba yake anamaongezi nae.....
hawakuweza kumgusa wala kumkamata Vida..kwa sababu ni mwiko kumgusa binti wa Mtemi...isipokuwa Mwanaume atakae kuwa Mume wake.....Vida akatoka ndani ya chumba hicho,, akazipiga hatua kuelekea kwa baba yake huku akilindwa kwaulinzi mkali......
Yule mkuu wa vijana hao akaingia ndani ya nyumba hiyo akamfuata Makala..akamtazama kwa macho ya huruma kisha akamuingelesha makala kwa lugha yao akimaanisha,,"Nasikitika sana kwa sababu unamasaa machache ya kuishi,,,alipomaliza kuongea hivyo akaondoka zake akimuacha Makala bado kaketi..lakini kitu kilichomshangaza zaidi Makala,,,alipomuona mkuu wa vijana wa kikololo akifunga mlango huo kwa nje.......Makala alistuka akajaribu kukumbuka Hayo maneno yanamaana gani? kwa sababu alishawahi kusoma historia ya jamii hiyo katika kitabu...hivyo alikuwa anaelewa baadhi ya maneno ua lugha hiyo.....ghafla akastuka akanyanyuka haraka..baada ya kukumbuka maana ya manenk hayo kwa kiswahili..macho yakamtoka akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi huku jasho linamtoka...akajisemea moyoni,,"Inamaana nitakufa!!!!????
*****************
upande mwingine alionekana Subi(mke wa Mtemi)
akijilaza kwenye kitanda kilichotengenezwa kwa miti kikiwa kimetandikwa kwa manyoya mengi ya ndege....na upande wa juu zikatandikwa ngozi mbili za mnyama simba.. Subi alikuwa akisubiri mumewe amalize kufanya matambiko ili amueze kile alichokuwa anakifanya binti yake wa pekee..
akajikuta amepitiwa na usingizi akasinzia kabisa bila kuongea chochote na mumewe..(Mtemi)
wakati huo alionekana Vida akiingia ndani ya nyumba...akamkuta baba yake(Mtemi) ameketi kwenye kiti baada ya kumaliza kufanya matambiko....Mtemi akasema,,kwa lugha yao akimaanisha,,"ulikuwa wapi?Binti yangu kipenzi!
nilikuwa na wasiwasi huenda umepatwa na jambo baya....kabla Mtemi hajamaliza kuingea,,akaja yule mkuu wa vijana wa kikololo..akatoa heshma kwa Mtemi kisha akasema,"tumemkuta kwenye ile nyumba tuliyomuhifadhi yule mtu tuliemkuta kule mstuni....
Mtemi akakasirika sana,,,akajisemea moyoni...yani huyu mwanaharamu anathubutu kumgusa binti yangu....hii ni Fedhea!! akaongea kwa ukali kwa kusema,,"nenda kamfunge kamba...na awekewe ulinzi wa kutosha ili asije akatoroka.....na itakapofika kesho asubuhi Anyongwe hadharani mlaka kufa ....
****************
upande mwingine kule mstuni alionekana Joshi akizipiga hatua za kikakamavu usiku huohuo akisonga mbele zaidi....aliweza kuona vyema kutokana na lile jicho la chui alilolipachika kwenye jicho baada ya kulilinyofoa.. jicho lake....
kwa sasa akawa na uwezo mkubwa wa kuona vizuri hata akiwa mbali....
alizidi kusonga mbele ....alitembea umbali mrefu mpaka pakakukucha.....kwa mbali akasikia kelele za watu wakiimba kwa kilugha akaamua kuelekea upande huo ambao kelele hizo zinapotokea......alipokaribia akaona watu wamekusanyika kumzunguka mtu aliyekuwa amesimama juu ya meza iliyotengenezwa kwa miti...huku kafungwa mikono yake kwa kamba. pia akamuona kijana mmoja wa kikololo akimvika kamba shingoni yule mtu aliyesimama juu ya meza hiyo...Joshi akatabasamu akazipiga hatua za haraka haraka kuwafuata watu hao....
Alionekana yule kijana wa kikololo akiendelea kuifunga kamba balabala juu ya mti ikitokea kwenye shingo ya Makala. watu wa jamii hiyo ya wakololo walikusanyika kushudia tukio hilo huku wakiimba nyimbo kwa lugha yao, Makala akavuliwa nguo zote nakubaki uchi wa mnyama tayari kwa kunyongwa....watu hao waliendelea kuimba kwa lugha yao huku wakipiga kelele wakimsubiri mtemi aje kutoa amri Makala anyongwe..
Ghafla ulionekana upanga mrefu uliorushwa kutokea msituni, upanga huo ulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye shingo ya yule kijana aliyekua anamfunga kamba Makala....akandondoka chini na kupoteza maisha papo hapo .,wale watu jamii ya wakololo wakashtuka na kutazama ule upande ambao ule upanga umetokea, wakamuona mtu mrefu mwenye sura ya kutisha akizipiga hatua kuja huo upande walipo .Wakaanza kurusha mikuki huku wengine wakirusha mishale, walirusha mikuki na mishale mingi mfululizo .
Mishale na mikuki iliingia kwenye mwili wa Joshi lakini Joshi aliichomoa na kuitupa chini pia alichomoa mikuki na kuirusha kule walipokuwepo wakololo.,
Wakati huo huo alionekana Makala akihangaika kujinasua kutoka kwenye kitanzi akafanikiwa kukata kamba zilizofungwa mikononi mwake ,akazua kitanzi (kamba iliyokua imefungwa shingoni mwake), akaanza kutimua mbio. Kutokana na mwili wa Makala kua mnene na kitambi ,Makala alipata wakati mgumu kukimbia kwa kasi akajikuta anadondoka mara kwa mara, kwa mbali alionekana Mtemi akiwa amesimama nje ya mlango wake macho yalimtoka akastaajabu kumuona Joshi.
***********
Upande mwingine kule msituni walionekana wale maaskari watano wakichimba shimo ndani ya kichaka hicho kwaajili ya kumzika mwenzao ....walipata wakati mgumu sana kutokana walikuwa hawana vifaa vya kuchimba shimo...wakaamua kuchimba kwa kitumia panga zao fupi..walizokuwa wamezifunga kwa mkanda...kwenye viuno vyao,huku wakiutoa udongo nje ya shimo hilo kwa kutumia mikono yao. iliwachukua masaa manne mfululiizo mpaka wakachimba shimo la urefu wa futi nne(4) walipomaliza wakamzika na kulifukia shimo hilo..wakatoka kwenye kichaka hicho na kuanza kutafuta njia ya kutoka kwenye msitu huo..walizipiga hatua huku macho yao yakitazama kwa tahadhari kubwa..na bunduki zao zikiwa tayari kupambana na chochote kitakachotokea mbele yao.....walitembea umbali mrefu sana..bila kupata uelekeo wa njia ya kutoka mstuni humo...wakaanza kupatwa na njaa....wakajikaza kwa kupoza njaa kwa kunywa maji yaliyokuwemo ndani ya vibuyu vyao vya plastiki....
*******************
Upande mwingine alionekana Michael akiwatafuta wenzake ili ahakikishe kama wapo salama..kwa sababu yeye ndio mkuu wa kikosi hicho,,,wakati huo,Michael alikuwa hajui kuwa kapoteza askari mwingine,,yeye aliamini bado wapo sita......akaendelea kuwatafuta wenzake.....aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote...akaanza kuhisi njaa...akaamua kuwinda angalau mnyama ili aweze kujipatia mlo.
haikuwa kazi ngumu kwa Michael kwa sababu alizaliwa katika familia ya Uwindaji...Baba yake alimfundisha kuwinda kwa kutumia mbinu mbali mbali za uwindaji....akachomoa upanga wake akakata Fito kadhaa (miti mwembamba sana) akachonga miti hiyo..ikatengeneza ncha kali....akachimba mashimo mafupi manne..akaichomeka miti hiyo..akachuna kamba za magome ya miti na kuifunga kwa kuivuta akafunga kamaba hizo kwenye mti mikubwa miwili..kwa kuegesha....akawa tayari katengeneza mtego wa kumnasa muama ueyote atakaye katiza eneo hilo..... akazipiga hatua na kujificha kwenye kichaka.......
**********************
Upande mwingine kule kwenye kijiji cha jamii ya Wakololo,,,hali ilikuwa tete...Joshi aliendelea kufanya mauwaji ya kikatiri bila huruma....
Mtemi....alipo ona watu wake wanauwawa akaingia ndani kufanya jambo fulani......akachukua mshale akaupaka dawa maalum kwenye ncha ya mshale huo... dawa hiyo ni sumu kali sana ya kichawi,,ya mila za Wakololo.... ambayo inauwezo wa kupenya kwenye Mzimu....hata kama Mzimu huo umevaa kiwiliwili cha Binadamu .......akachukua upinde akazipiga hatua akatoka upande wa nje....
Wakati huohuo Joshi aliendelea kuwaangamiza wale vijana wa Jamii ya wakololo...akachukua ule upanga wake kwa kuuchomoa kutoka kwenye shingo ya yule kijana alimchoma kwa kuurusha upanga huo.....akaanza kuwafyeka shingo zao vichwa vikaruka kando....Joshi aliuwa watu wengi kwa muda mchache...
wakololo waliobaki wakaanza kutimua mbio na kutokomea mstuni..baada ya kuona mambo yamekuwa magumu.......
Mtemi alionekana akutafuta sehemu nzuri ya kujificha ili aweze kuufyatua mshale huo kutoka kunako upinde huku akiwa ametulia.......na kulenga shabaha kwa umakini mkubwa ili mshale huo uingie katikati ya kifua cha..Joshi.
akafanikiwa kupata sehemu ya kujificha vyema...akachukua ule upinde akaweka mshale na kuuvuta vyema...akawa tayari kwa kuufyatua....lakini alikuwa akisubiri Joshi ageuke ili afyatue mshale huo kifuani mwake...
Ghafla Joshi akageuka ili kutazama nani kabaki ili amuangamize.........
Mtemi akavuta upinde huo kwa nguvu zake zote akauachia mshale huo............
Joshi akauona mshale huo..akaukwepa na kutimua mbio akatokomea Mstuni...
aliweza kuuona mshale huo kwa haraka kutokana na lile jicho la chui alilolipachika kwenye sehemu ya jicho lake....aligundua kuwa mshale huo ni hatari kwa uhai wake,,ndio sababu iliyomfanya atimue mbio...
Mtemi alikasirika sana...kwa sababu ile dawa aliyoipaka kwenye mshale...haipatikani kwa urahisi..inaweza kumchukua miaka arobaini(40) kuitengeneza dawa hiyo...na inatumika mara moja tu..bila kurudia...vinginevyo itamlazimu utengeneze dawa nyingine.....kwa miaka arobaini(40).
Akaangaza angaza macho yake huku na kule..akasikitika sana kuona viwiliwili vingi vya maiti zisizokuwa na idadi....huku vichwa vimekatwa na kudondoka aridhini..damu nyingi ilitapakaa katika kijiji hicho cha jamii ya Wakololo.
Baada ya lisaa limoja kupita walionekana baadhi ya wakololo waliokimbia kwenda kujificha kwa ajili ya kuokoa maisha yao,,,wakitokea mafichoni kurudi kule kwenye kijiji chao....
*****************
Upande mwingine alionekana Michael bado akiwa amejificha ndani ya kichaka,,akiendelea kusubiri mawindo yake...ule mtego umnase mnyama ili aweze kujipatia kitoweo....alisubiri kwa muda mrefu bila kuona dalili yoyote ya mnyama kuja upande huo! akakata tamaa akaamua kusonga mbele kuwatafuta wenzake...
wakati huo huo walionekana wale maaskari watano wakizipiga hatua za tahadhari huku macho yao yakitaza kwa umakini mkubwa......ghafla wakasikia vishindo vizito vya miguu ikikimbia.....wakaanza kushambulia kwa kufyatua Risasi mfululizo kwenye ule upande ambao vishindo hivyo vilisikika....
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni