DHAMANA (28)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kipindi hichi ndiyo Hamis naye alikuja kuungana nasi baada ya kumuoa Salma na alipata nyumba ya kukodisha Usagara akakaa huko na tukawa tukifanya kazi pamoja, miaka miwili baadaye Ally akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Usagara ilibidi tumuhamishie nyumbani kwa Hamis ili awe karibu na shule asome vizuri.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Tuliendelea kuchapa kazi kwa kipindi hicho hadi tukawa na mafanikio kidogo yaliyoniwezesha kuhama Mpirani nikaja kuishi Chumbageni baada ya kuweza kukodi nyumba nzuri iliyoniwezesha kukaa vizuri na familia yangu. Ally alimaliza kidato cha nne alikuja kuungana na sisi Chumbageni na kuifanya familia yetu iwe na furaha zaidi kwani Jamadin alikuwa amekaa karibu na Ally mtu anayeelewana naye sana.
Mwaka huo aliomaliza Ally kidato cha nne ndiyo mwaka ambao mambo yalibadilika kwa nna ya kustajabisha sana, vitega uchumi vyetu vilianza kuyumba na kupungua katika namna ya kustajabisha sana hadi ikafikia tukawa na kitega uchumi kimoja tu ambacho nacho kilitekea na moto katika mazingira ya kutatanisha. Hali hiyo ilitufanya tuanze kufanya kazi kama waajiriwa ili tuokoe familia zetu na tuweze kusogea hatua kadhaa kimaendeleo, tulifanya kazi na kulisha familia zetu pamoja na kulipa pango la nyumba na hakukuwa na pesa nyingine yoyote iliyobaki tuseme tutatumia kuanzisha shughuli nyingine.
Mambo yalipoanza kuzidi kuwa mabaya wote kwa pamoja tuliweka kikao nyumbani kwa Hamis na tukashauriana tuende kumuona mtaalam aliyetusaidia kumuondoa Faimu kijijini huenda akatusaidia cha kufanya ili tuweze kukomboka katika balaa hili, siku iliyofuata wote kwa pamoja tulienda Duga maforoni kwenda kuonana na mganga wetu aliyetufanyia dawa miaka kadhaa iliyopita.
Safari hiyo ya kwa mganga ndiyo iliweza kubainisha tatizo la kukwama kwa mambo yetu, tulimkuta mtoto wake yule mganga ambaye ni Sauti ya radi ambaye alitutajia tatizo kubwa la kuharibika kwa shughuli zetu niliambiwa lipo kwangu na tulihitaji utatuzi basi nikubaliane na sharti la kutoa kile kinachofanya kuwe na kssumba katika mipango yetu. Nakumbuka vizuri maneno ya mganga Sauti ya radi aliniambia, "mtoto unayelea ndiyo kikwazo cha kukwama kwa matatizo yenu na kama mkitaka mfanikiwe basi yule mtoto anatakiwa atolewe sadaka katika eneo alilozaliwa na baadaye utakuja kupata mtoto wa pili wa kike ndiye akikua utajri utazidi na hata wenzako watatajirika pia".
Kweli ilikuwa ngumu sana kukubali lakini nilipoelezwa juu ya nguvu kubwa za maajabu alizonazo yule mtoto kiasi kwamba ameweza kutambua uchawi nilimuwekea mama yake hadi nikampata. Mganga alienda mbali akanitajia uajabu wa huyo kama siamini niende nikamkate kidogo mkononi mwake nijifanya ni bahati mbaya halafu niangalie kitakachotokea, siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimechanganywa na masharti ya mganga na nikaagana na wenzangu nikawaambia kesho tutajua cha kufanya kingine.
Sikutaka kuamini mambo ya yule mganga nimtoe kafara mtoto wa pekee niliyekuwa naye wakati hata wa pili bado sijajaliwa, nilipingana na suala hilo lakini nilitaka nijaribu vile alivyoniambia mganga ili nione itatokea vipi. Majira ya alasiri siku hiyo nilikuja na mpira wa upepo wa ndani ya baiskeli nikawa na panda kipende cha mti kinatumika kutengeneza manati, nilimuita Jamadin nikamuambia anishikie miandae mipira kwa ajili ya manati nataka kuipeleka shamba itumiwe na banu yake.
Jamadin alinielewa mapema ingawa ndiyo kwanza alikuwa ana miaka mnne, alishika nilivyomuelekeza na nilianza kukata ule mpira wa baiskeli na nikajifanya nimekosea nikamkata na kiwembe na damu ilimtoka lakini alitulia kimya tu. Kitendo hicho kilinichanganua na nikajikuta naangalia pembeni nitafute walau kitambaa nizuie damu isitoke, niliangaza macho pembeni nikakosa kitambaa na niliporudisha macho sehemu niliyomkata Jamadin nilijikuta nikishtuka hadi nikarudi nyuma kwa uoga. Jeraha lile nililomkata na kiwembe sikuliona na niliona hakukuwa na jeraha sehemu yoyote katika mkono wake, Jamadin yeye alikuwa ananitazama kwa dharau tu nilivyokuwa natetemeka baada ya kutoona jeraha nililomkata na kiwembe.
"Uahajua ulichotaka jua?" Aliniuliza hivyo na nilipokaa kimya aliondoka bila kunisemesha chochote na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuanza kumuogopa yeye na pia nikajikuta nipo tayari kwa sharti alilonipa mganga Sauti ya radi. Siku iliyofuata nilienda kuonana na wenzangu mapema iwezekanavyo na nikawaeleza juu ya kila kitu nilichokishuhudia na nilikuwa tayari kumtoa Jamadin kwani siyo mtoto wa kawaida, siku hiyo tulienda kwa sauti ya radi na tukaambiwa vitu vilivyokuwa vinahitajika kwa ajili ya kafara ya Jamadin.
Ilihitajika jeneza dogo jeusi linalolingana na urefu wa Jamadin, damu ya mwisho wa mwezi wa mwanamke, chupa ya ujazo wa nusu lita yenye mfuniko na kaniki nyekundu mita moja na visu saba. Vitu vingine tuliambiwa vitapatikana hapo kwa mganga na kafara hiyo ambayo ilipangwa kufanyika usiku wa kuamkia siku ya ijumaa ambayo ni keshokutwa yake na mikakati ya kumnasa Jamadin tuliambiwa ianze. Mganga Sauti ya radi alisema atatusaidia katika kumfunga Jamadin asibaini kitakachokuja kutokea. Baada ya kupewa hayo mahitaji wote tulienda kuyatafuta siku hiyohiyo ya jumatano na ilipofika jioni tulikuwa tumeshapata kila kitu, siku iliyofuata tulipanga mikakati ya kumnasa Jamadin katika mikono yetu bila yeyote kutambua ili twende tukamtoe kafara mipango yrtu ifanikiwe.
Ili kutimiza azma yetu ya mtoa kafara Jamadin tuliamua tumtumie Ally kwani ndiyo njia rahisi ya kumnasa Jamadin, siku hiyoida ya alasiri nilimuagiza Ally Makoroea kwa makusudi na Jamadin aliomba kwenda na nikamruhusu kwani hiyo ndiyo njia ya kumnasa. Huko Makorora tulikuwa tumeandaa vijana wa kukodi waliokuwa wanatumia gari aina ya volkswagen tuliyomuazima tajiri mmoja wa jijini Tanga enzi hizo aliyeitwa Brown ambaye ni chotara kwa sasa ni Marehemu, tajiri huyu mwanae wa kiume ndiye alikufa kule Duga Maforoni wakati nyumba za kampuni ya Hamid zilipoungua na pia mjukuu wake smbaye namtambua kwa jina la James alikufa mulemule.
Vijana hao walifaniliwa kuwateka Ally na Jamadin na kuondoka nao ambapo njiani Ally alipigwa kisogoni akazirai akatupwa kando ya reli mita chache kutoka katika mzunguko wa Kwa Minchi majira ya usiku, kupotea kwa Jamadin na Ally nyumbani kwangu ilikuwa ni huzuni sana kwa mke wangu lakini kwangu mimi ilikuwa ni kawaida kwani nilikuwa najua kila kitu. Tulikusanyika nyumbani wanaume wote huku mimi nikionekana kulia sana na nilibembelezwa hadi nikanyamza ndipo tulipoanza kujadiliana kimaigizo nini cha kufanya, baada ya mjadala wanaume wote sita tulikubaliana tuongie mtaani kumtafuta Jamadin na Ally na wake wote wakakaa nyumbani kwangu wakimbembeleza Farida
****
Tuliwaacha wake zetu na matumaini hewa ya kurudi wakiamini tulikwenda kumtafuta kumbe tulikwenda kufanya kitu kingine tofauti na kumtafuta mtoto huyo, haikuwa safari ya kwenda kumtafuta Jamadin kama walivyokuwa wakifikiria bali tulikuwa tunaenda kumalizia shughuli yetu tuliyoambizana na mganga Sauti ya Radi ikamilike siku hiyo. Sehemu ya kwanza baada ya kutoka nyumbani kwangu ilikiwa ni Kisosora upande wa ufukweni mwa bahari ya Hindi jirani na kichaka kimoja, hapo tuliwakuta wale vijana wakiwa na Jamadin waliyemfunga kamba ngumu pamoja na kitambaa mdomoni ili asipige kelele.
Walitukabidhi Jamadin kwani tulikuwa tushamalizana nao kila kitu na ilikuwa ni kuagana baada ya kukabidhiana tu, hicho ndicho kilifanyika hapo na sisi tukaianza safari ya kuekea mpirani ambapo tulifika majira ya saa ya tano usiku tukiwa na asusa yetu. Ilipokaribia saa sita mganga alianza kuandaa mazingira ya kuanza ikiwa ni pamoja na shimo kubwa kuchimbwa katika eneo la sebule ambalo ndiyo hapa tumekaa, baada ya kazi hiyo kukamilika alituambia tulizunguke shimo hilo tukiwa na kisu mkononi kila mmoja ambavyo vilikuwa vimefungwa vipande vya kaniki nyekundu upande wa kwenye mpini wa kushikia.
Mganga alianza kazi yake kwa kupiga manyanga huku akiimba nyimbo alizozitambua yeye na baada ya muda upepo mkali sana ulisikika ulivuma kama kimbunga kuizunguka nyumba tuliyomo, upepo huo uliendelea kuvuma hadi mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni hapo uliokuwa umefungwa ulifunguka kwa nguvu sana. Ulikuwa ni upepo wenye kuogopesha lakini mganga alituambia tusitetereke na lile duara letu kulizinguka shimo tulilolichimba tuache uwazi upande unaotazamana na mlango, Hamis na Falzal ambao walikuwepo katika upande huo walijisogeza pembeni kwa kutusukuma sisi na sisi tulisogea ili waweze kutimiza maelekezo ya mganga ya kupisha njia.
Upepo ule mkali uliendelea kuvuma na ulizidi kutuogopesha sana lakini tulijikaza kisabuni kama watoto wa kime, ulizidi kuvuma na hatimaye ukaingia ndani ukapita pale kwenye upenyo wa duara letu ukaingia hadi kati ya shimo tulilochimba ukajenga sura ya mtu kwa kutumia vumbi la kimbunga ambalo ndilo liliingia nalo. Kitendo cha kuona umbile la mtu katika upepo huo tulijikuta tukitamani kukimbia ilikuwa inaogopesha sana sana lakini mganga alitusihi tusikimbie na tufanye kile atakachotuambia, mganga kwa kitendo cha upesi alimwaga ile damu ya mwezini ya mwanamke kulizunguka shimo hilo na ule upepo ukawa unajaribu kutoka ndani ya eneo lililozunguahiwa damu lakini ulishindwa kwani ulipokaribia mpaka wa ile damu ambayo ni ya Shemeji Salma ulirudi huku sauti isiyoeleweka kama ya popo aliyejeruhiwa ndiyo ikawa inasikika kutoka kwenye ule upepo.
Mganga baada ya kuhakikisha ule upepo umeshindwa kuivuka ile damu ya Mwezini alituamrisha tuchome visu vyetu kwa pamoja katika sehemu ya kifua na ya mgongo ya umbo la mtu lililotengeneza na upepo huo kwa kutumia vumbi jingi lililosababishwa na huo upepo, wote kwa pamoja tulichoma visu vyetu kwemye huo upepo ambavyo vilitupa hisia ya kwamba tumetoboa kitu hadi makelele ya popo aliyejeruhiwa yakssikikakwa nguvu kwenye ule upepo kisha ukazama ndani ya shimo kwa mara moja.
Hapo ndipo mganga akambeba Jamadin aliyekuwa kafungwa kamba akiwa anafurukuta aweze kutoka lakini alishindwa kutokana na kamba ngumu alizokuwa amefungwa, alimuingiza ndani ya shimo hilo kisha akaliingiza lile jeneza tulilolileta ndani ya shimo pamoja na chupa. Alimlaza Jamadin juu ya jeneza kisha akatuamuru kila mmoja amchanje mara sita kwa kutumia kisu alichonacho mkononi, sote tulifanya ambapo Jamadin alitoa ukelele wa maumivu lakini hatukumjali hata kidogo mpaka tulipomaliza kumchanja ndipo tulipoanza kuona ajabu jingine lilitokea katika mwili wa Jamadin baada ya yeye kutanua mdomo apige kelele tulipomaliza kumchanja lakini kelele hazikutoka zaidi ya kutoka mwanga mweupe ulioingia ndani ya chupa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni