TANGA RAHA (14)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Nikajinyanyua kiuvivu vivu kisha nikaingia bafuni nikapiga mswakii na kuoga na kurudi chum-bani na kuvaa nguo kwa ajili ya kwenda kazina kwani hata hamu ya kukaa ndani ya nyumba niliyo hamia tayari ilishaanza kunipoteSASA ENDELEA...
“Eddy natai saa hizi unakwenda wapi?”
“Nataka niende kazini”
“Saa hizi?”
“Kwani ni saa ngapi?”
“Saa nne na nusu asubuhi”
“Haina tabu nitakwenda hivyo hivyo”
Ok basi njoo unywe chai”
Nikakaa mezani na kuanza kunywa chai aliyo iandaa Hilda huku kichwani kwangu nikiwa na mawazo ya kumfikiria Olvia Hitlar kwa vituko anavyo nifanyia
“Mbona unaonekana kuwa unamawazo?’
“Nipo kawaida”
“Kawaida? Eddy japo sijakaa na wewe kwa muda mrefu ila nimesha kuzoea hiyo hali yako sio ya kawaida”
“Kawaida nizoee”
“Asubuhi nilikwenda sokoni nikanunua vitu muhimu vya ndani na kama utahitaji matunda yapo kwenye friji”
“Sawa”
“Mmmmm mbona unanijibu shoti shoti au kwasababu nimejipendekeza kwako?”
“Hapana”
Nikamaliza kunywa chai na kuchukua begi langu lenye laptop na baadhi ya vitabu na kulivaa mgongoni
“Mchana nikupikie nini?”
“Chochote ila leo uende kwako”
“Sawa nitakupikia mapishi ya kihindi ukija wewe mwenyewe utafurahi”
“Sawa”
“Nikupeleke kwa gari?”
“Hapana nitapanda daladala”
“Mmmm haya kazi njema”
Kabla sijatoka Halda akanishika mkono na kunipiga busu la mdomoni kisha akainiachia na ni-kaelekea kwenye kituo cha daladala nikapanda na sikutaka kusemeshana na mtu hadi nikafika sehemu ninayo shuka na kumuomba konda kusimamisha gari na mimi nikashuka na kulipa pesa yake anayo ihiyaji.
Nikafika shuleni na kuingia moja kwa moja ofisini na kuwafanya waalimu wengine kunishangaa kwani hawakutarajia kuniona katika siku ya leo
“Eddy si unaumwa?”
“Kidogo najisikia vizuri nikaona ni bora nije kazini kuwajibika”
“Aaisee ningekuwa ndio mimi nimepewa ofa kama yako ningekaa mpaka ninenepe”
Mwalimu John alizungumza na kuwafanya waalimu wengine kucheka kwa furaha kwani kwa jinsi alivyo mwembamba ni vigumu sana kwa yeye kunenepa kwa likizo fupi
“Sir John una kipindi kidato cha nne ‘A’?”
“Ndio ninavyo viwili vya historia”
“Basi nakuomba kidogo nikawafundishe Physics”
“Sawa hakuna tatizo”
Nikachukua vitabu vyangu vya somo la Physics nikiwa natoka mlango wa ofisini nikakutana na Madam Recho akanipandisha na kunishusha kisha akaachia msunyo wa chini chini nikampote-zea wala sikusemeshana naye na nikaeelekea katika darasa la Kidato cha nne.Wanafunzi waka-nisalimia kama kawaida
“Monitor hembu nenda kaangalie form four B kama hawana mwalimu waambie wale wano so-ma Physics wote waje”
Monitor akatoka na kuniacha nikiwa ninapiga mistari ubaoni kwa kutumia chaki kujiandaa kwa kufundisha somo hilo linalopendwa na wanafunzi wachache.Kilicho nishangaza ni wale wanafunzi wasio soma somo hilo kubaki darasani kwani tumezoea kuwaona katika vipindi cha Physics hutoka darasani na kwenda kujisomea.
Wanafunzi wa kidato cha nne B wakaja wote hata wale waiso soma somo hilo na nikabaki nimeshaangaa
“Walio kosa viti wakachukue viti vyao na haraka tuje tuendelee na somo hili la leo”
Wanafunzi wakafanya kama nilivyo waagiza na baada ya muda darasa likawa limejaa vizuri na wakaanza kunisikiliza kwa umakini.
Kila nikijaribu kuiweka akili yangu sawa ili niandike vitu vinavyo husiana na somo la Physics nikajikuta ninashindwa na taratibu nikaanza kuisikia sauti ya Olvia Hitler kwenye akili yangu akinielezeea kitu cha kufanya
“Leo naona tuiache Physics kidogo na tuangalie somo la history kama mtu utakuwa na sehemu ya kuandika notce basi fanya hivyo.Hata nyuma ya daftati wewe andika
“Sir hata nyuma ya daftari la Physics?”
“Ndio”
Akilini mwangu nikaanza kupata picha ambayo Olvia Htler akaniomba niielezee kama ninavyo iona
“Kulikuwa na vijana wawili mmoja akiitwa Janet na mwengine akiitwa Eddy……Hawa vijana walikuwa wamependa katika chuo kimoja kinaitwa HALLTON.Katika hali ya kawaida vijana hawa wanaonekana ni binadamu wa kawaida japo wanauzuri wa kuvutia machoni mwa watu wengine….Janet yeye alikuwa ni jamii ya malaika kutoka kwa Mungu ila mama yake ni binadamu wa kawaida ila baba yake ni malaika.
Ila kwa upande wa huyu Eddy yeye alikuwa ni jamii ya kishetani na babu yake alizaa na shetani na kuweza kutengeneza familia yenye watoto wenye nguvu za ajabu
Kwa upande wa Eddy aliweza kumshawishi Janet ambaye alikuwa ni mpenzi wake kufanya naye vitu vya ajabu vilivyo weza kumfanya Janet akiuke katika yale mambo muhimu aliyo taki-wa kuyafanya kama mtu wmema.
Kitendo hicho kilizidi kumuudhi muumba wa mbingu na nchi mpaka ikafikai hatua akaamua kuingamiza dunia.Ila kwa upande wa Eddy akisadiana na Dareen binti mwenye asili ya kishetani huku kukiwa na binti mwengine anayeitwa
Minaele ambaye naye ni jamii ya shetani toka katika falme nyingine ya kishetani inayoitwa Golden Kingdom na kwapamoja wakawa na lengo kubwa la kuweza kuiokoa dunia isiangamie jambo lililokuwa gumu na ikapelekea Eddy kuingia kuzimu hii ni baada ya kumsukuma shetani aliye jipa jina la Dulah
Dunia yote ilaanza kuwaka moto huku Janet akichukuliwa na wazazi wake ambao ni Malaika japo Janet alikuwa na mwenye dhambi.Kwa usiri wa hali ya juu Janet aliweza kuitunza mimba alitopewa na Eddy na akajifungua mtoto wa kiume ambaye kila jisi muda na wakati ulivyozidi kwenda ndivyo jinsi navyokuwa.
Na mukumbuke kuwa Eddy ana asili ya kishetani na Janet anaasili ya Kimalaika.Janet akampa mtoto wake jina la Hitler na akawa ni miongoni mwa malaika walio na nguvu nyingi kupita wengine wote.Hitler akazidi kumsumbua mama yake juu ya alipo baba yake ndipo mama yeke akaamua kumueleza ukweli wa nini anachopaswa kukifanya katika kumfungua baba yake alipo katika bwawa kubwa la moto linalo lindwa na
Malaika wenye nguvu na hakuna anayeweza kudhubutu kutoka kwani waliomo ndani ya bwawa hilo wamefungwa na minyororo mikubwa na migumu kupita maelezo.Kuna siku Hitler alizungumza na mama yake katika maficho ya siri yaliopo mbinguni kiasi kwamba ni vigumu kwa wengine kusikia wanacho kizungumza
‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU
“Mazungumzo kati ya Hitlaer na mama yake ambaye ni Janet yaliendelea kwa usiri mkubwa hu-ku mama yake akimfundisha mbinu ambazo zitamsaidia mwanae katika kuikamilisha kazi ya kumuokoa baba yake.Hitler alijipanda vizuri na kutokana ni mjukuu wa miongoni mwa Malaika wakubwa mbinguni aliweza kutumia kigezo hicho kushuka duniani bila ya kuhojiwa maswali mengi na walinzi wanao linda dunia ambayo ipo katika hali mbaya ya kuuguzwa moto.
Hitler akaaanza kufanya uchunguzi wake kwenye shimo kubwa la moto liitwalo KUZIMU lililo kusanya idadi kubwa ya watu walio tenda maovu,Ila katika kuzimu nako kumegawanyika madaraja ya mateso ambayo yapo saba.
Na kila waliopo kwenye daraja moja wanatofautiana kwa adhabu na waliopo kwenye daraja la pili hivyo hivyo na kuendele mbele kiasi kwamba ma-tendo yako ndio yanakuchagua uingie kwenye daraja lipi unalo stahili kuhukumiwa.
Hitler akaendelea kufanya uchunguzi wake katika magereza yote saba ila hakufanikiwa kumuona baba yake ambaye kwa jinsi mama yake alivyo muelekeza sio rahisi kwake kushindwa kumtambua ila gafla Hitler akiwa kuzimu……”
“Sory Sir Eddy muda wa kipindi chako umeisha”
Madam Zena alizungumza huku akiwa ameshika vitabu vya somo la Kiswahili jambo lililo pele-kea wanafunzi kuanza kuzomea wakikataa asiingie
“Jamani tutamalizia hii story yetu kesho”
“Ahhhh Sir EDDY endelea bwanaaa Kswahili bongo akawafundishe mabasha zakee”
Sauti mmoja ya kiume ikitokea nyuma ya darasa ilisikika na kumfanya madama Zena kuchungulia mlangoni huku sura yake ikiwa imekasirika
“Mwana idhaya nani aliye zungumza hayo maneno?”
“Si ninawauliza nyinyi watoto mulio laaniwa na wazazi wenu.Msio na haya mafirahuni wakubwa nyinyi munajua maana ya basha……..Ehhhhh au munavyo jiona nyinyi humu ndani kuna mwanaume aliye kamilika nyote si mashogaa”
Madam Zena alizidi kutokwa na maneno ya kejeli hadi ikafikia kipindi wanafunzi wa kiume wa-kaanza kuzungumza chini chini na neno lililo sikika kutoka nyuma ya darasa walipo kaa wana-funzi wengi wa kiume ni
“Shoga baba yako aliyekuzaa”
Nikabaki nimeshika mdomo kwani kwa jinsi madam Zena alivyo mweupe wa kujichubu taratibu nikamuona sura yake ikitawali na wekundu kwa mbli ulio tokana na hasira
“Nasema nyote tokeni nje mupige magoti”
Wanafunzi wote wakakaa kimya wakisikilizia nani aanze kwenda nje kupiga mogoti ila kadri muda unavyo zidi kwenda hakuna aliye simama kwenda nje
“Monitres nenda kamuite Headmaster na mwalimu wa nizamu”
“MONITRES MSALITIIIIIIIIII”
Monitres baada ya kuisikia sauti hiyo ya wezake ikambidi akae kwenye kiti chake na kujikausha kimya na kumfanya madam Zena kuzidi kuchanganyikiwa na hasira ikazidi kumpanda
“Na wewe Malaya ndio umekataa kunyanyuka kisa hao washenzi wezako si ndio?”
“Mimi sio Malaya”
“Kama sio umalaya ni nini kinacho kufanya usiamshe hicho kidude chako uende nilipo kuagiza kuna mwanaume anaye kupak**?”
Madam Zena akazidi kumfokea mtoto wa watu ambaye kiumbo ni mdogo sana kiasi kwamba huwezi kumfananisha na maneno anayoyazungumza Madam Zena
“Zena hembu kausha basi hawa ni watoto usizungumze maneno machafu kama hayo”
“Tena wewe mwana hizaya nilikuwa ninasubiria uingize hilo domo lako lililo kosa haya kumbe wewe ndio unawatuma hawa watoto ili walate jeuri si ndio?”
“Hapana Zena ila heshima ni kitu cha bure na tambua mujibu wako wa kazi ni upi ila si kuwatu-kana watoto wawatu”
“Nenda kule………….Hanisi mkubwa wewe uliye na Jogoo asiye wika anakazi ya kujikunyata ka-ma mbwa jike anayesubiri kupandwa na mbwa dume”
“ZENA……… ZENA……..ZENA”
“Zena jina langu mtoto wa pwani niliye fundwa na kujua jinsi ya kumkatikia yule anaye hitaji kuliko wewe mwanaume suruali”
Machozi ya hasira taratibu yakaanza kunimwafika huku mwili mzima ukitetemeka na kunifanya nitazame chini na sikutaka wanafunzi waitadhimini sura yangu ya hasira.Darasa zima limekaa kimya wakimsikiliza Madam Zena anavyo ropoka maneno machafu kiasi kwamba yanachafua masikio
“Wakisema wanaume watoke na wewe utatoka mwanaume unaye kimbia vita na kufungia watu milango kwa nje”
“ZENA FUNGA BAKULI LAKOOOO
“Heheee eti nifungea bakuli langu hata huyo anaye nit*** haniambii nifungee bakulii lan-gu…..KANITANGAZEEE MWANAUME SURUALI WEEE”
Meza ya mwanafuzi aliyepo mbele yangu nikainyanyua kwa hasira na kuirusha kwa nguvu na kutua kwenye miguu ya Madam Z ena na kumuangusha chini na kuwafanya wanafuni wote kushangaa huku wakimtazama Madam Zena akipiga kelele za kulalamika kuvunjwa mguu.Nikatoka darasani kwa hasira na kwenda moja kwa moja ofisini na kukaa kwenye kiti changu huku ninalia kwa hasira na kuwafanya waalimu wengine kunishangaa
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni