DHAMANA (27)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"Sasa kama hakuna haja ya wafuatilia basi Farida na Faimu nao wamependana haina haja ya wafuatilia waache na mapenzi yao na pia usitegemee nitaumia kwa jinsi kaka yangu anavyolazimisha kupenda kwa Farida ikiwa hatakiwi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Tena ukirudia tena nitongoza kwa njia hii nitakushtaki kwa kaka ili amuambie Hamis wakujue tabia yako ambayo waifanya kwangu" Ndiyo maneno yaliyotoka kinywani kwa Ally baada tu ya kumuambia kuhusu hiyo habari hadi nikawa najiona kama nimepungua umri na umbo kutokana na maneno yake jinsi alivyoniumbua.
Nilikubali kwa Ally nimeshindwa kwa siku hiyo labda nijaribu kwa mbinu nyingine kabisa tofauti na ile ili niweze kumpata kwani alinivutia sana, niliamua sasa kwenda kuifanya njia yangu ya pili ya kwenda kumuambia Hamis ambayo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani alichukizwa sana na kusikia Faimu ana mahusiano na dada yake na taarifa hiyo ilifikishwa kwa Shafii na mipango hiyo ya kwenda kwa mganga ili kumkomoa Faimu ndipo ilipoanza".
Salma aliweka kituo kikuu katika kusimulia kwake na hadi muda huo mzee Buruhan alikuwa akimtazama kwa hasira sana kutokana na kuujua ukweli wa tabia yake, watoto wake nao walioneshwa kuwa na mshangao hasa wa tabia aliyokuwa anafanya mama yao kwani hawakutegemea kama ataweza mambo kama yale.
Upande wa Bi Farida baada ya Salma kumaliza kusimulia kilichompata tayari hasira dhidi ya shoga yake kipenzi zilikuwa zipo juu na mawazo ya urafiki nae yalikuwa yameshatoka kichwani mwake, alimtazama wazi kwa macho yaliyojaa chuki kuu iliyoongezewa na machozi yenye uchungu kutokana na masikio yake kupata hiyo habari ya kuwa rafiki yake aliyempenda na kumuamini amekuwa akimzunguka kwa miaka mingi bila ya yeye mwenyewe ingawa alimuamini sana na kumthamini.
Ama kweli kikulacho kinguoni mwake kama waliozaliwa toka awali walivyonena na rafiki yako ndiye adui yako kama ambavyo waliozaliwa toka walivyotoa maana ya msemo wao huo waliounena, ama kweli rafiki anaweza akawa siyo rafiki kama ambavyo Salma alivyokuwa akifanya kwa Farida haikustahiki aitwe rafiki kwani kafanya yasiyostahiki kufanywa na anayeitwa rafiki kwani ni usaliti mkubwa sana alioufanya.
Baada ya kisa hicho mhusika wa aliyeita hapo familia zote ambaye ni mzee Mahmud alikuwa akimtazama kila mtu aliyepo eneo hilo katika uso wake ili kujua hali zao zipo vipi waliposikia simulizi hiyo, alizungusha shingo yake iliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kwa kila mmoja aliyepo eneo hilo huku akiwa mithili ya mtu anayechambua fikira za mtu zilizomo ndani ya ubongo wake na mwishowe akayatuliza macho kwa rafiki yake kipenzi wa tangu, ujana na hadi wanazeeka pamoja. Mzee Mahmud alimtazama rafiki yake hadi alipobaini katambua kama anamtazama ndipo akafungua kinywa chake, "mzee mwenzangu umesikia mambo ya watoto wetu hayo? Je una lolote la kusema kabla sijaendelea na kinachofuata?"
Mzee Buruhan alipoulizwa hilo swali alimtazama Shafii kwa umakini kisha akamuuliza, "Shafii hivi Farida ni nani yako?"
"ni mke wangu baba" Shafii alijibu akiwa ameinamisha uso wake chini kutokana na aibu aliyonayo kwa baba yake baada ya mabaya yake kubainika.
"Kwa kigezo kipi Farida mkeo we mwana? Aliridhia kwa moyo wake wakati unaenda kutoa posa au kizizi chako ulichokichukua huko Maforoni ndiyo kilimfanya aridhie?" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali wa wastani na kusababisha Shafii atazame chini kwa aibu kutokana na kitendo alichokifanya kwani kilikuwa cha aibu sana tena amekieleza mbele ya watoto.
"Wajukuu samahanini sana kama nitakuwa nimekosea na pia nitakuwa sijaongea kauli nzuri kwa mujibu wa maadili yetu mbele yenu nyinyi. Ila lazima niseme ukweli juu ya hili, alichokifanya huyu ambaye ni mjomba kwa wengine na pia ni baba kwa mwingine ambaye yupo hapahapa ni sawa na kumuingilia mwanamke akiwa amelewa hivyo ninaona alikuwa anabaka na hayupo katika ndoa. Sina la ziada mzee mwenzangu" Mzee Buruhan aliongea maneno yaliyozidi kumuumiza Shafii na pia kumtia sibu mbele ya mtoto wake pamoja na wapwa zake, maneno hayo yalimfanya Zalabain azidi kuwa na hasira na mama azidi kulia kwani alikuwa amekosewa haswa na kosa kubwa lenye kujaza maudhi tele kwa kiumbe yoyote mwenye uhai na aliyejaliwa akili na matamanio.
Mzee Mahmud naye alisikitika sana hulu akimtazama Shafii na Salma kwani alijua fika wamefanya ujinga mkubwa sana ambayo utawafanya waumie na wajute kwa muda mfupi tu na hawatapata bahati ya kuusafisha ujinga huo tena katika dunia hii kwani wakati wake ulipita wakati jambo hilo wanalifanya. Walikuwa wamepoteza muda wao mwingi katika matumizi mabaya yasiyofaa na walifanya kosa pasipo kusahau kubwa hawataweza kulisahihisha tena hilo kosa, kwani muda wake ulishapita tayari hivyo matumizi yao mabaya ya muda wao kipindi cha nyuma ndiyo yalimfanya mzee Mahmud awasikitie kila akiwaangalia.
Giza nje ya eneo hilo lilikuwa tayari lishaumeza mwangaza mdogo wa muda wa magharibi ambao waliukuta kipindi wanaingia eneo hilo, nuru yote ilishapotea tayari na kiza kizito kikawa kimelimeza eneo lote kwa nje kutokana na uwepo wa miti na mapori katika eneo la jirani na hiyo nyumba. Majira hayo yalimfanya mzee Mahmud aendelee na utaratibu aliouweka kwa haraka ili usiku mnene usiwakute wakiwa eneo hilo, na kutokana na msjira hayo ilimbidi aseme "Shafii sasa endelea kusimulia ulipoanza mahusiano yako na Farida hadi mnaishi kwa pamoja".
Sauti ya mzee Buruhan ilifika mapema zaidi hata ya robo sekunde tu tangu azungumze katika masikio ya Shafii ambaye naye alinyanyua kinywa chake na kusimulia, "Baada ya Farida kuwepo katika mikono yangu na kuwa msichana nilikuwa nikikutana naye kimwili kupunguza mihemko ya ujana na pia nilifanya hivyo ili tu nikija kumkosa niwe tayari nimeshatumia mwili wake kwani hilo ni jambo la fahari sana kwa kijana kama mimi, sikuwa na imani na dawa hizo na niliamini dawa niliyomfanya anipende itaisha tu kutokana na kiwewe cha kupendwa ghafla na sikuwa ninaamini kabisa kama nitakuja kuendelea kukaa naye.
Nilianza kuingiwa na imani ya kuendelea kukaa naye baada ya Hamis kunishauri nipeleke posa nyumbani kwao nimuoe moja kwa moja kuliko kusababisha mimba mapema, jambo hilo nililikubali kwa mikono miwili na nikaona hiyo ndiyo njia inayofaa ili kumfanya Farida awe wangu kabisa na hata kama Faimu akija kujua ajue tayari amemkosa Farida na si mali yake tena. Kwa mara ya kwanza katika ujana wangu nilijivika ujasiri na kumueleza baba yangu juu ya suala hili na yeye alifurahishwa na uamuzi wangu wa kwenda kuposa akiniambia tayari nilishakuwa mkubwa na hilo ndiyo jambo la maana nimeamua kama kijana anayejitambua, baba yangu alienda kumueleza mzee Jumanne ambaye ndiye baba mzazi wa Farida ambaye aliridhia kwa mikono miwil hilo suala kutokana na utiifu nilionao kwake hapo kijijini.
Taarifa hiyo ilipelekwa kwa Farida ambaye alikubali na furaha yangu ikazidi na hapo ndipo nikazidi kuamini ile dawa ya mganga ambaye ni baba mzazi wa mzee Sauti ya radi ilifanya kazi na inaendelea kufanya kazi na wasiwasi wa kumoksa Farida sikuwa nao kabisa, baada ya muda mfupi baba yangu aliweka kila kitu sawa ndos ikafungwa na tukayaanza maisha yetu katika nyumba ya baba yangu iliyokuwa ipo shambani kwake huku wazazi wa pande zote mbili wakituahidi kututafutia makazi yaliyobora kwa ajili yetu.
Maisha yetu na ndoa na Farida yalikuwa ya furaha kwa kipindi cha mwaka wa kwanza na katika kipindi hicho nilikuwa tayari nishaanza kufanya shughuli ili nipate kipato kwa ajili ya familia yangu na mke wangu maisha yetu yaende mbele, mwaka wa pili wa ndoa yetu ulipoingia Farida alianza kuweweseka usiku na alipoamka asubuhi alikuwa mchovu sana hali iloyozidi kunipa wasiwasi sana na ikanilazimu niende kwa baba mzee Mahmud akanipa dawa ambaye nilimpatia dawa ambayo ilimsaidia Farida sana akawa hapatwi tena na hali hiyo, baada ya Farida kupona hilo tatizo haikupita hata muda mrefu akashika ujauzito ambayo ulinifanya niwe na furaha sana na hata wazazi wa pande mbili walijawa na furaha baada ya kuwapa taarifa hiyo.
Furaha ya wazazi baada ya Farida kupata ijauzito ilionekana wazi baada ya kutupatia zawadi iliyotufurahisha zaidi, wazazi wa pande zote mbili walijenga nyumba kubwa hadi ikaisha bila sisi kutambua na walikuja kutukabidhi baada ya kuwapelekea taarifa ujauzito na wakatuambia ndiyo sehemu ya pekee itayotufaa kuanzisha familia yetu. Nyumba yenyewe ndiyo nyumba hii ambayo tumo wote hivi sasa ambayo ilitufanya mimi na mke wangu kuhama kule kijijini na kuja kuishi hapa Mpirani nikiwa na mdogo wangu Ally, tuliyaanza maisha mapya kwa furaha sana na mdogo wangu Ally tayari alikuwa yupo shule ya msingi akiwa yupo ukingoni kumalizia elimu hiyo.
Miezi tisa ilipitimia Farida alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya nzuri ambaye alizidi kuongeza furaha ya ndoa pamoja na furaha ya wazazi wetu ambao walikuja kututembelea na wakapata bahati ya kumuona huyo mtoto aliyelepekea furaha yetu izidi, mtoto huyo tulimpa jina la Jamadin ambalo ni jina la babu yangu mzaa mama ili jina hilo zuri lisiweze kupotea bila kupatikana mrithi wake ndani ya dunia hii kama ilivyo kawaida ya jamii zetu kurithisha watoto wao majina ili tu jina liwepo na liendelee kuwepo. Jamadin alikuwa ni mtoto mchangamfu sana na aliyefanya familia yetu iwe na furaha kuputiliza, matendo yake ya tangu utoto yalikuwa ni yenye kufurahisha na ndiyo maana familia yetu ilizidi kuwa na furaha.
Kipindi hicho tayari Ally alikuwa ameshamaliza elimu ya msingi na alikuwa anasubiri majibu ili aweze kuendelea na elimu ya sekondari ambayo ilikuwa ikionekana na hadhi kubwa kama mtu akiisoma, muda huo wa kusubiri majibu ndiyo muda ambao Ally alikuwa akiutumia kucheza na Jamadin hadi akawa amemzoea sana kuliko hata mimi niliyekuwa nashinda kwenye mihangaiko Makorora na kurejea nyumbani jioni sana.
Baada ya mwaka mmoja kupita tayari Ally alikuwa sekondari na ndugu zangu wengine wote walikuwa wapo Tanga mjini tukifanya shughuli pamoja baada ya kuoa kila mmoja, furaha ya kuwa karibu na ndugu zangu ndiyo ilizidi maradufu kwani kazi tuliifanya kwa umoja na kuzidi kujiingizia kipato kwa ajili ya familia zetu ambazo zilitegemea sana uchapaji kazi wetu ili ziweze kujipatia chakula na mahitaji mengine muhimu. Kipindi hichi ndiyo Hamis naye alikuja kuungana nasi baada ya kumuoa Salma na alipata nyumba ya kukodisha Usagara akakaa huko na tukawa tukifanya kazi pamoja, miaka miwili baadaye Ally akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Usagara ilibidi tumuhamishie nyumbani kwa Hamis ili awe karibu na shule asome vizuri.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni