Notifications
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…
  • THE NIGHTMARE (5)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa…
  • THE NIGHTMARE (4)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.“unanipiga mimi?...utaona!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Aliongea Karim na kuondoka huku analia.*****************************Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa…
  • Fumanizi la Mchepuko Mwizi😂 | Comedy
    Mume amefuma viatu vya mchepuko wa mke wake mlangoni lakini akakosea kuingia ndani kabla aweke umakini kwenye hivyo viatu mwisho wa siku akaibiwa na vyake😂Hili tukio lazima lichukuchekeshe sana hata kama ulikuwa haujataka kuchekaItazame kisha nipe like na ukinipa maoni kwenye comment nitashukuru sanaUsisahau kubonyeza Subscribe kama haujajiunga na fungua #ChekanaZephiline kupata video zangu zote ambazo zipo mtandaoniNashukuru sana kwa wewe ambaye unanipa nguvu ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri…
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…

AISEE KUMBE RAHA (17)

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA SABA
Lakini kabla hata sijafika mbali baada ya kushuka katika daladala na kuelekea nyumbani kizunguzungu cha ghafla kikanikumbaa na kunijikuta nikijishika kichwa baada ya kuanza kuhisi maumivu lakini kabla hata sijaendelea ghafla ukungu mzito ukatanda katika mboni zangu nakujikuta nikishindwa kujizuia na Haikuchukua hata dakika nikadondoka mzima mzima mpaka chini na kuzimia Hapohapo...............

SASA ENDELEA...
Nikuja kushtuka na kukuta watu wengi wakiniangalia nikiwa chini ya Ardhi nimelala ambapo baada ya kuangaza angaza Macho nilikuja kugundua kuwa yalikuwa ni maeneo yale yale nilipodondoka baada ya kukumbuka mapema nini kilichonitokea kwa sababu mara ya mwisho nilikuwa nijisikia maumivu ya kichwa.Watu wengi waliokuwa wakiniangalia wengi wao nilikuwa nawajua kwa sababu ilikuwa ni mtaani kwetu ambapo watu wengi walikuwa wananifahamu kwa sababu mtaani pia nilikuwa najichanganyaga na vijana wenzangu ambao wote tulikuwa tunacheza nao Mpira.

"Vipi pablo mwanangu umedondoka kama mzigo yani maana wana walipoona walikuwa wakata kukusaula nguo zote lakini Baada ya kuingilia tukaja kugundua ndio wewe vipi kwani una nini." Yalikuwa ni maneno ya moja kati ya rafiki yangu ambaye nilikuwa nimezoeana naye sana ambaye aliponiambia vile haraka nikajisachi mifukoni mwangu nakuanza kutafuta simu Yangu ambayo kwa bahati nzuri niliona na nilipoitoa Nikakutana na Messeji mia na tano zikiambatana na Missed call mia tatu ambazo hata siku moja sikuwahi kupigiwa namna ile.Hofu ikaanza kutanda kabisa katika moyo wangu ambao ulianza kudunda haraka sana si kawaida kuona hali ile ilitosha kabisa kuniaminisha kuwa hali ilikuwa si nzuri basi na Suzan atakuwa amevujisha kabisa picha zile ambazo alinipiga wakati nilipokuwa nimelala baada ya kufanya naye mapenzi.

"Mhhh huu msala sasa." Nikajikuta nikisema kwa nguvu na kusababisha marafiki zangu waanze kuniuliza maswali mengi ambayo hakuna hata moja nililolijibu.Haraka nikanyanyuka na kujikuta vumbi kisha kwa mwendo wa haraka haraka nikaenda Nyumbani ambapo Baada ya kufika ndani nikajikuta Nikipigwa na butwaa kubwa baada ya kuona gari likiwa nje gari ambalo lilitosha kuniaminisha kuwa Baba yangu alikuwa amerudi kutoka safarini ambapo Mara nyingi huwa anaondokaga na kwenda katika Biashara zake.

"Aisee au nisirudi Nyumbani niondoke."nikajikuta nikiongea mwenyewe kama chizi baada ya kufika karibu na nyumbani na kukuta tayari kuna ugeni ambao sikuwa na huitaji kwa wakati ule.Hakika sio siri baba yangu alikuwa ni mtu tofauti sana maana mara nyingi alikuwa si muongeaji bali alikuwa ni mtekelezaji mkubwa wa kitu ambacho anahamua mwenyewe kufanya.Hakika kufika pale kulikuwa hakuna jinsi kabisa kwa sababu hata mwili wenyewe ulikuwa umeshachoka kabisa na wala sikuwa na ujanja wa kwenda sehemu nyingine.Nikachukua simu yangu nakuangalia saa nikakuta na saa ambayo ilikuwa ikionyesha wakati huo saa mbili kasoro usiku taratibu nikapiga hatua na kuukaribia mlango wa nyumbani na taratibu nikaufungua bila ya uoga na kuzama ndani ambapo nilikutana uso kwa uso na baba ambaye aliachia tabasamu pana kisha na mimi sikuwa na budi nikamsogelea na kwenda kumkombatia huku nikionyesha sura ya furaha ambayo haikuwa ya furaha kutoka moyoni ilikuwa ni furaha kumpumbaza tu Baba ambaye alionekana kabisa kunikumbuka.

"Shikamoo baba."
"marhaba kijana wangu mwenye jembe langu ninalo litegemea."
"Daaa mimi mzima baba kabisa yani nimekumiss sana baba yangu."Nilijitutumua kuongea na Baba ambaye aliniletea zawadi zawadi nyingi kama Nguo na viatu ambavyo alikuwa ametoka navyo huko alipotoka congo.Baada ya salamu kupita na kuongea Mengi mimi na baba na kujumuika na mama ambaye alimficha vitu vingi baba ambaye aliulizia kabisa majanga niliyoyafanya lakini mama alisema hakuna matatizo kabisa.baada ya mazungumzo marefu ambayo nilitamani yaishe na kweli yaliisha mwanaume nikazama ndani na moja kwa moja nikaenda kuoga na nilipomaliza nikaenda kujumuika na Mama na baba kula kisha baada ya kushiba nikarudi ndani chumbani kwangu na kwenda kuchukua ile simu yangu nakuangalia je zile messeji mia na tano na missed call zilikuwa ni za nani kwa sababu haikuwa kawaida mimi kutumia messeji nyingi namna ile.

"Mwanangu kuanzia sasa sio rafiki yangu kweli shoga wewe unajiuza facebook na kujitangaza shoga pablo."Hakika ilikuwa ni messeji ya kwanza kuifungua na kujikuta nikipigwa na butwaa la ajabu hakika sikutegemea na nilipoangalia alikuwa ni nani alikuwa ni rafiki yangu mpendwa ramadhani ambaye mara nyingi alikuwa karibu sana na mimi.Hofu kubwa ikitanda katika moyo wangu na haraka nikawasha internet na kukutana na messeji kibao ambazo zilinichanganya.Picha zangu hakika zilizambaa kwa kasi sana picha ambazo nilipigwa pasi na ridhaa yangu na mpigaji alikuwa si mwingine bali ni suzan ambaye kwa hakika sikutegemea kuwa yeye angeweza kunifanyia inshu namna ile inshu ambayo nilimfanyia catherini.Hakika
Moyo wangu haukutaka kabisa kuamini kuwa nilikuwa nimeingia choo cha kike na kilichozidi kuniuma sana ni baada ya karibia marafiki zangu wote walinitumia picha zile ambazo zingine zilikuwa ni picha ambazo suzan alinipiga na kuonyesha kuanzia Mgongoni mpaka katika makalio yangu.Hakika nilijikuta nikianza kulia sana Baada ya kugundua haikuwa ni kusambaza tu niliposoma messeji zingine walikuwa ni baadhi ya wanaume ambao walikuwa wananitaka na nilipoangalia tena ndipo nilipogundua kuwa suzan alikuwa amefanya kama nilivyomfanyia mimi catherini baada ya kwenda katika mtandao wa instagram na facebook na kuandika.

"Mimi jamani nauza atakayehitaji anitafute kwa Namba hizi."yalikuwa ni maneno yalioandikwa facebook na instagram huku aliyeandika aliambatanisha na namba yangu ya simu hali ambayo ilisababisha nichanganyikiwe kabisa.nikiwa na mawazo mengi huku nikiendelea kulia ghafla simu yangu ikaita na nilipoangalia ilikuwa ni Namba ngeni nikajikuta nikiipokea kwa hasira na kumsikiliza ni nani aliyekuwa akipiga.

"Halooo."
"Halooo wee nani."Nikajikuta nikipandwa na hasira zaidi baada ya kusikia sauti ya kiume hali iliniaminisha kuwa Mpigaji alikuwa ni Mwanaume.
"Aaaaa bibie mbona mkali hivyo."Bila ya kutegemea jamaa akaniita bibie na kusababisha nigande kumsikiliza na kuona kama Ndoto vile ambayo nilikuwa naota tu na inaishia palepale.
"Bibie mimi na pesa sana nimeona picha zako facebook mimi ndio ugonjwa wangu halafu nina miela Mengi kama vipi nambie Unauza Kwa ngapi."Hakika asikuambie Mtu dunia imeisha jamaa alivyokuwa anaongea kama alikuwa anaongea na mwanamke hasira kali zikanipanda na kujikuta nikirusha ile simu yangu na kwenda kutua katika ukuta na kuvunjika papohapo.Hasira kali dhidi ya Suzan zilikaanza kuibuka maradufu hakika alifanya kitu ambacho sikumfanyia yeye bali ni shoga yake hakika asikuambie Mtu wanawake wengine hawa sio watu wazuri.sikuamini kabisa kama suzan alikuwa amenidharirisha kuliko nilivyomfanyia catherini ambaye nilimfanyia vile baada ya kutaka kwenda kutoa umbeya ambao ulikuwa hauna faidi kwake.
"Aaaaaaaaaa Hakia mungu sikubali Nitamuuua huyu suzan Tena kwa mikobo yangu pumbavu!!!"...

Maneno ya hasira kali yakanitoka huku nakujikuta nikikunja Ngumi kwa hasira kali huku machozi yakiendelea kunititirika Mashavuni.Hakika akili yangu ikabadilika kabisa na kujikuta nikidhamiria kabisa kuwa patakapokucha basi lazima niende kumuua suzan huku mipango yangu ya kichwa ikiniambia niende kumuua chiku kwa kumchomoa na kisu.Hakika siku ile usingizi ulipaa na kujikuta mpaka saa tisa nikiendelea kulia kwa sababu ya uoga ambao je Mama akigundua na kuona zile picha za mwanae nikiwa vile je nitamwambiaje au je Baba yangu ambaye alikuwa ndio kwanza amerudi safarini halafu anakaribishwa na siku zake za kupumzika nyumbani na picha zile ambazo hakika sura yangu katika picha zingine zilionekana vizuri na hakika ubora wa picha zile na zilivyokuwa zinaonekana wala hakukua na njia ya kujitetea je itakuaje baba akijua.Kilichozidi kuniogopesha ni ukali wa baba yangu ambaye yeye alikuwa hana Maneno mengi zaidi ya kutekeleza Adma ya kitu ambacho kutamjia tu kichwani mwake basi yeye alikuwa tayari kabisa kufanya maamuzi.Baada ya kuwaza sana usingizi ukaja kunichukua katika mida ya saa kumi na moja alfajiri ambao kama inavyokuwaga unaweza ukakesha siku nzima lakini ukajikuta ukipatwa na usingizi kukaribia na Asubuhi.Kama ilivyoada Mwanaume nikalala kabisa usingizi mzito kabisa ambao ukanisahaulisha kwa muda majanga ambayo yalikuwa yametokea ambayo kwa hakika hakukuwa na jinsi gani ya kupona.

"Pablooo pablooo weee pablo."nikiwa katika usingizi mzito ambao ulikuwa mtamu kabisa kupindukia ghafla nikashtushwa na sauti kali ya baba sauti ambayo ukali wake na uzito wa sauti ile ndio ulitosha kabisa kunifanya niamke huku nikiwa na usingizi usingizi ambao ulikuwa bado kabisa haujaisha.Haraka nikanyanyuka na kupiga hatua kwenda kufungua mlango lakini nikajikuta nikikanyanga kioo ambacho kilinikata na nilipoangalia kile kioo kilikuwa ni kioo cha simu yangu aina ya galaxy simu ambayo niliipasua kwa bahati mbaya baada ya kukumbwa na hasira za juu baada ya kupigiwa na mwanaume ambaye eti alikuwa akinitaka mimi mwanaume mwenzake baada ya kuona picha ambazo nilipigwa na mwanamke ambaye katika maisha yangu sikumtegemea kama angeweza kunifanyia vile kisa rafiki yake ambaye aligombana naye na Mama yake alitaka kumshushia kipigo.Baada ya kujikata haraka nikanyanyua ile simu ambayo ilivunjika vunjika na kuitupa chini ya uvungu ili baba asiione Maana angeiona angeuliza Maswali mengi ambayo yangesababisha mimi kukosa la kujibu.Baada ya kumaliza kuitupa ile simu ambayo ilikuwa haitamaniki na nilitoa laini yangu tu taratibu nikaufungua Mlango ule na kukutana uso kwa uso na baba ambaye alikuwa makini kuniangalia.

"Jiandiae sasa hivi twende Mjini na naomba uniazimie simu yako Mara moja."
"Daaa baba sasa hivi sina simu ile nilidondosha ikavunjika kwa hiyo kwa sasa sipo hewani."Nilimuambia baba maneno yale ambayo aliyapokea kwa kicheko kikali sana huku akiniangalia na taratibu akanishika bega langu.
"Sasa Pablo mbona jana nilikuwa nakupigia simu ilikuwa inaita na tena usiku ule mida ambayo ndio umerudii."Baba akanitandika swali lilosababisha moyo uanze kudunda na kujikuta nikikwepesa Macho kumuangalia maanake Baba alikuwa mtu wa kudadisi sana Alikuwa hapendi sana kuniacha na niwe nafanya mamlaka mwenyewe licha ya kuwa nilishafika age ya kijana mkubwa ambaye alitakiwa kabisa kuondoka nyumbani lakini yeye mpaka muda huo alikuwa akipenda sana kunichunguza na kunidadisi.

"Aaaa....mmm....m..bona...labda ssss..io yangu Maana laini yangu mbona ipo kwenye drooo pale."Niliongea kwa kutetemeka huku nikimuangalia baba ambaye wala hakutaka tena kuendelea na hali ya kunidadisi.
"Usijali basi baba nimerudi mjini kila kitu kitakuwa sawa twende mjini na simu nitakununulia jiandae haraka."Baba yangu alihitimisha na kusababisha hofu iondoke kwa pale kisha akaondoka pale mlangoni wa chumba changu na kuniacha nikimsindikiza kwa macho.Haraka nikaingia ndani na kubadilisha nguo kisha nikaenda chooni na kwenda kuoga haraka haraka na nilipotoka kuoga nikakutana na Baba ambaye tayari yeye alikuwa ameshajiandaa.

"Fanya haraka my boy muda huu watoto wasikuhizi bana fanya haraka."Baba akanisisitizia na mimi nikamuelewa nikazama na kwenda kuvaa nguo zangu za mtoko na nilipomaliza haraka nikatoka na kuongoza na mzee mpaka katika gari yake na wote tukaingia katika gari safari ya kwenda mjini ikaanza na kumuacha mama ambaye alisisitizia kuwa alikuwa akihitaji zawadi ya sisi tunaotoka.Safari ya kwenda mjini ikaanza safari ambayo tulikuwa tukipiga stori nyingi na mzee ambaye alinipa na simu yake na kuanza kunihadithia habari za michepuko wake.Hakika mzee wangu alikuwa ni zaidi ya rafiki yangu ambaye mara nyingi alikuwa akipenda sana kuniambia Mambo yake ya siri ambayo kama angeyajua Mama basi ndoa yao ingevunjika aliniaminii mimi kama mtunza siri wake na hakika hata sikumoja sikuwai kumuangusha kwa hilo neno tuliyokuwa tunayazunguza hakuwai hata siku moja kuyasikia kwa Mama na jambo lile lilisababisha azidi kunipenda mno.
"Haya niambie kijana wangu maana uhandsome wako balaa una demu hivi maana tukiongea mada hizi huwa unapendaa kukaa kimya."Baba akanitandika swali ambalo likanifanya nicheke huku nikiwa bize na simu yake ambayo nilikuwa nimeingia internet naangalia habari za mchezo.
"Daa mzee nimeachana naye kwa ugomvi mkubwaa."
"Anhaaa pole kawaida bia kama imeisha tingisha weka na nyingine."Mzee aliniambia kimasihara na kusababisha wote tucheke huku mzee akiendelea kuendesha gari lake kuiangalivu wa hali ya juu.Tukiwa tunakaribia kufika mjini ghafla simu yake ikaingia ujumbe mfupi ambao ulipoingia Baba akaomba simu yake lakini nikajifanya kama sijasikia haraka nikaingia uwanja wa messeji na nikakutana na messeji ambayo presha iliyokuwa kama imesahaulika ikaja tena kwa kasi ya ajabu.
"Mzee nimeona picha za kijana wako ni shoga au maana anajitangaza ana uza mzee kizazi chako shidaa eeee."Yalikuwa ni maneno ambayo yalitumwa kwa njia ya messeji na mtu ambaye baba alimsave kwa jina la mwenyekiti wa kamati haraka nikaingia na kuifuta messeji ile lakini ili namaliza tu baba akaninyang'anya na kuchukua simu yake.

"Nilisikia mlio wa messeji ni nani huyo aliyetuma messeji harafu mbona siioni."Baba akaniuliza swali na kujikuta nikimdanganya eti nilikuwa nimeenda katika sehemu ya mlio tukafika mjini na baba akaenda kupaki gari lake katika sehemu ambayo yakupakia magari kisha tukaanza kwenda madukani ambapo baba akaanza kwenda katika maduka ya simu ambapo Bila ya kutegemea akaninulia simu mpya aina ya samsung ambayo kwa hakika wala sikutegemea.Ghafla simu ya baba ikaita akaipokea na kuipeleka sikioni.
"Aaaaa wapi mmmh chuoni anhaaa pablo anahitajika na Mimi hapo chuoo sasa hivi anhaa sawa sawa nafika hapo nipo naye."yalikuwa ndio mazungumzo ya baba na ile simu mazungumzo yaliosababisha nishtuke baada ya kumaliza baba kuongea na ile simu akaniangalia kwa Macho ya umakini sana.
"Oya pablo kuna nini huko chuoni maana sijakuuliza hata kimoja kuhusu chuoni kwako nimelipa millioni moja na nusu sasa fanya ujinga uone na twende sasa hivi hapa kama kurudi tutarudi siku nyingine."mzee akamaliza kuongea na haraka tukarudi katika gari letu na tukaanza kuondoka kuelekea chuoni ambapo hapakuwa mbali na mjini.Baada ya kufika tukashuka kwenye gari baada ya kwenda kupaki gari letu katika sehemu ya kupakia magari chuoni kisha nikaanza kumuongoza Baba kuelekea kwa mkuu wa chuo ambaye ndio alimpigia simu baba.Hofu ikaendelea kutanda sana na hakika nilikuwa najificha ficha nisionekane kirahisi na watu ambao wengi wa marafiki zangu pale chuoni walikuwa wameshaziona picha zangu zile.kwa bahati nzuri tukaingia hadi katika chumba cha mkuu wa chuo bila hata ya mimi kuonekana na watu ambao walikuwa wakinifahamu.kama ilivyo desturi baba na yule mkuu wa chuo wakasalimia vizuri tu lakini niliposalimia mimi na yule mkuu hali ilikuwa tofauti mkuu yule alikuwa akiniangalia kwa jicho kali sana hadi baba akashangaa kwa sababu aliona kila kitu.
"Haina haja hata ya kuwakaribisha licha ya kuwa nimewaita sasa basi twende moja kwa moja katika lengo la kukuita kuwa kwanza mwanao tumeshamfuta hapa chuoni."
"Whaaaaaaaaaaaat.!!!!

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA NANE

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
4 Aisee Kumbe Raha Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni